Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 18.04.2020: Mane, Neymar, Pogba, Buffon

leo


Sadio ManeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane(Aliye na mpira) huenda akahamia Real Madrid

Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane huenda akahamia Real Madrid, kwa mujibu wa mchezaji mwenzake wa Senegal Keita Balde, ambaye pia aliongeza kuwa Mane, 28, Pia anaweza kusalia Anfield "milele". (AS, in Spanish)
Barcelona inatarajiwa kuwasilisha ofa ya kumnunua mshambuliaji nyota wa Brazil Neymar, 28, kutoka Paris St-Germain.
Miamba hao wa soka wa Uhispania wako tayari kuwajumuisha Samuel Umtiti, Ousmane Dembele na Jean-Clair Todibo katika mkataba huo baada ya hali yao ya kifedha kuathiriwa na Jana la coronavirus. (Mundo Deportivo, in Spanish)

NeymarHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBarcelona itawasilisha ofa ya kumnunua mshambuliaji nyota wa Brazil Neymar, 28, kutoka Paris St-Germain

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 27, anatarajiwa kutia saini mkataba mpya Manchester United na huenda akawa kiongozi wa klabu hiyo, kwa mujibu wa mwandishi wa michezo wa Uhispania Guillem Balague. (Express)
Kipa wa muda mrefu wa Juventus Gianluigi Buffon, 42, amekubali kurefusha mkataba wake katika klabu hiyo. Hii itakuwa msimu wa 19 kwa mtaliano huyo Turin. (Tuttosport, in Italian)

Paul PogbaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionPaul Pogba, 27, anatarajiwa kutia saini mkataba mpya Manchester United

Fiorentina ipo tayari kumuuza Federico Chiesa anayenyatiwa na Manchester Unite, lakini inasema kiungo huyo wa miaka 22- hataki kuondoka klabu hiyo. (Sun)
Borussia Dortmund ilimtaka mshambuliaji wa Uingereza Mason Greenwood, 18, Manchester United ilipowasiliana na klabu hiyo kutaka kumnunua winga wake Jadon Sancho, 20. (ESPN)
Arsenal huenda ikapoteza nafasi ya kumsajili Layvin Kurzawa kutoka Paris St-Germain. Beki huyo wa Ufaransa wa miaka 27, alikuwa tayari kuondoka PSG kwa mkopo wa bila malipo lakini sasa mkataba wake huenda ukarefushwa. (Sport)

KurzawaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJe Arsenal itafanikiwa kumsajili Layvin Kurzawa kutoka Paris St-Germain?

Hertha Berlin wamewasilisha mkataba wa awali wa kutaka kumnunua winga wa Paris St-Germain Julian Draxler. Arsenal pia wamekuwa wakimfuatilia kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani wa miaka 26. (Foot Mercato, in French)
Mkufunzi wa Atletico Madrid Diego Simeone amewasiliana na mke na ajenti wa mshambuliaji wa Paris St-Germain Mauro Icardi, Wanda Nara, kuhusu uwezekano wa kumnunua nyota huyo wa Argentina. Icardi, 27, kwa sasa yupo Inter Milan kwa mkopo kutoka PSG. (Tuttosport, in Italian)

Mauro IcardiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji wa Paris St-Germain Mauro Icardi

Arsenal, Chelsea na Everton wanajaribu kumsaini beki wa Lille Mbrazil Gabriel, 22. (ESPN)
Inter Milan wanataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Ufaransa Anthony Martial, 24, wakimkosa Lautaro Martinez kutoka Barcelona msimu huu. (Gazetto Dello Sport, in Italian)

Anthony MartialHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionInter Milan kumsajili Anthony Martial wa Manchester United wakimkosa Lautaro Martinez kutoka Barcelona

Hatahivyo, Barcelona hueda wakawapoteza wachezaji kadhaa msimu wa joto kutokana athari za janga la coronavirus. (ESPN)
Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Diego Costa, 31, huenda akaondoka Atletico kwa uhamisho wa bure mwisho wa msimu huu. (Marca)

Tetesi za Soka Ijumaa

Everton huenda wakamsajili kiungo wa kati wa Aston Villa Muingereza Jack Grealish, 24, wakipata nafasi. Blues kwa sasa wanamtaka mshambuliaji wa Gremio na Brazil, Everton Soares, 24. (Sky Sports)
Wakala wa mshambuliaji wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez, 28, amewasiliana na Manchester United kuhusu uwezekano wa uhamisho wa nyota huyo msimu huu. (Sport via Metro)

James Rodriguez
Image captionManchester United huenda ikamsajili mshambuliaji wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez msimu huu

Liverpool wanafanya mazungumzo na ya kumsajili kiungo wa kati wa Milan na Croatia Marcelo Brozovic,27. (Libero via Express)
Real Madrid wanampango wa kusalia na Luka Jovic ambaye pia analengwa na Arsenal. Mshambuliaji huyo wa Serbia wa miaka 22, amechezea Real mechi moja pekee msimu huu. (Sport via Sun)
Barcelona inamtegemea Philippe Coutinho,27, msimu ujao, amesema mkufunzi Quique Setien. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye yuko Bayern Munich kwa mkopo, amehusishwa na tetesi za uhamisho kuenda Chelsea ama Tottenham. (Evening Standard)

Philippe CoutinhoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBarcelona inamtegemea Philippe Coutinho(Kushoto) msimu ujao

Manchester United wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsaka beki wa Birmingham wa miaka 16-Muingereza Jude Bellingham katika mkataba wa awali wa thamani ya £35m. Chelsea na Borussia Dortmund pia wanamng'ang'ania Bellingham. (Sun)

Post a Comment

0 Comments