Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 25.04.2020: Aubameyang, Giroud, Osimhen, Ndombele, Werner, Ruiz

Chelsea wanafuatilia kwa karibu hali ya Pierre-Emerick Aubameyang katika Arsenal wakiwa na matumaini ya kumchukua mshambuliaji huyo wa miaka 30 raia wa Gabon msimu huu.(ESPN)
Barcelona na Inter Milan pia wako makini na Aubameyang, huku klabu hiyo ikiamini kuwa the Gunners watalazimika kumuuza kwa bei ya chini msimu huu. (Telegraph)
Arsenal wamesitisha kwa muda mazungumzo ya makataba na Aubameyang na wako tayari kuwasikiliza wanaomtaka mshambuliaji huyo. (Mail)
The Blues wamefanya mkataba na klabu ya Lille ya Ufaransa kumuhusu Mualgeria Victor Osimhen, 21 anayecheza katika safu ya mashambulizi . (Le10Sport - in French)
Olivier GiroudHaki miliki ya pichaEPA
Chelsea wamekubali kurefusha mkataba kwa mwaka mmoja zaidi na mshambuliaji Mfaransa Olivier Giroud, mwenye umri wa miaka 33. (Di Marzio - in Italian)
Barcelona wanataka kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele, mwenye umri wa miaka 23, kutoka Tottenham,
Na wametoa pendekezo la sehemu ya mkataba wa kubadilishana wachezaji ambayo itamuwezesha kiungo wa kati -nyuma wa Ufaransa Samuel Umtiti, mwenye umri wa miaka 26, na kiungo wa safu ya nyuma-kulia Mreno Nelson Semedo kuhama baina ya timu.(Sky Sports)
Chelsea wanajiandaa kubaki na mlindalango Muhispania Kepa Arrizabalaga, 25, licha ya kuwa makini na mchezaji wa kimataifa wa Italia anayechezea kikosi cha AC Milan Gianluigi Donnarumma, mwenye umri wa miaka 21. (Mail
Paris St-Germain wametoa ofa kwa kiungo wa kati wa Argentina Angel di Maria, mwenye umri wa mkiaka 32,arejee katika Manchester United,
pamoja na winga Mjerumani Julian Draxler, mwenye umri wa miaka 26 kama sehemu ya mpango wa kubadilishana mkataba kwa ajili ya kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 27. (Calciomercato, via Sun)
kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 27Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 27
Mkurugenzi wa mchezo wa klabu ya RB Leipzig Markus Krosche hajapokea maombi yoyote ya uhamisho aliyoyapokea kumuhusu mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner wiki katika kipindi cha za hivi karibuni licha ya taarifa zilizoripotiwa kwamba kumekuwa na timu zinazomtafuta kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 kama Liverpool na Barcelona. (Goal)
Manchester City, PSG na Juventus zote zinamsaka kiungo wa kati wa Lyon Houssem Aouar, mwenye umri wa miaka 21. (RMC Sport - in French)
Mmiliki wa klabu ya Napoli Aurelio De Laurenti ametaja beiya kianzio ambayo anaweza kumuuza kiungo wa kati Mhispania Fabian Ruiz,mwenye umri wa miaka 24, huku Manchester City wakiwa makini kusaini mkataba.(Teamtalk)
Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 20, kutoka Borussia DortmundHaki miliki ya pichaEPA
Image captionJadon Sancho, mwenye umri wa miaka 20, kutoka Borussia Dortmund
Kiungo wa kati wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, mwenye umri wa miaka 19, anasema angependa klabu yake isaini mkataba na Muingereza mwenzake Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 20, kutoka Borussia Dortmund. (Mirror)
Everton wamewasiliana na Barcelona juu ya namna wanavyoweza kumpata difenda Mbrazil Emerson mwenye umri wa miaka 21, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika kikosi cha Real Betis. (Sport - in Spanish)
The Toffees wameonyesha nia ya kumchukua kwa mkopo mchezaji mwenye haiba ya juu Mbrazili Philippe Coutinho, mwenye umri wa miaka 27. (Sport - in Spanish)
Roma wako tayari kumpa ofa ya kwa mkataba wa miaka mitatu offer a three-year Mshambuliaji wa mbele wa Napoli raia wa Ubelgiji Dries Mertens. (Corriere dello Sport, via Goal in Italian)
Muhispania Dani Ceballos, ambaye ni kiungo wa kati anayecheza kwa mkopo kutoka Real MadridHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMuhispania Dani Ceballos, ambaye ni kiungo wa kati anayecheza kwa mkopo kutoka Real Madrid
Mchezaji wa Arsenal mwenye umri wa miaka 23-Muhispania Dani Ceballos, ambaye ni kiungo wa kati anayecheza kwa mkopo kutoka Real Madrid, anasema amehakikishiwa hali yake ya baadae kimchezo. (Evening Standard)
Aston Villa na Crystal Palace wanamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Fabio Borini.
Muitalia huyo mwenye umri wa miaka 29-kwa sasa anachezea klabu ya Hellas Verona. (L'Arena, via Birmingham Mail)

Post a Comment

0 Comments