Tetesi za soka Ulaya Jumanne 28.04.2020: Pogba, Lingaard, Sancho, Dembele ,Coutinho, Kean

Manchester United wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 27, na kiungo wa kati wa England Jesse Lingard, 27, kumnunua Sancho. (Sun)
Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmunda anasema "amenyamaza " kuhusu hatma ya baadae ya Jadon Sancho. Winga huyo wa England, 20, amehusishwa na tetesi za kuhamia Manchester United. (Sport1 - in German)
Mshambuliaji wa Everton Moise Kean, 20, amehusishwa na tetesi za kuhamia Napoli.
Mtaliano huyo huenda akachukuliwa hatua za kinidhamu na Everton kwa kukiuka muongozo wa serikali wa kukabiliana na coronavirus mapema wiki hii. (Corriere dello Sport - in Italian)
Moise KeanHaki miliki ya pichaAFP
Wachezaji nyota wa Barcelona Philippe Coutinho, 27, na Ousmane Dembele, 22, wako tayari kujumuishwa kwa mkataba wa kubadilishana wachezaji msimu huu. (Telegraph - subscription required)
Chelsea walimtaka Coutinho lakini sasa wanamnyatia kiungo matata wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 20. (Athletic - subscription required)
Arsenal wamewasilisha ofa ya £43m kumnunua kiungo wa kati wa Atletico Madrid na Ghana Thomas Partey, 26. (Express)
Thomas ParteyHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Liverpool wanapigiwa upatu kumsajili mshambuliaji wa Lille Victor Osimhen, 21, ijapo kuwa Leicester na Chelsea pia wanamng'ang'ania raia huyo wa Nigeria . (Le Foot Mercato - in French)
Arsenal wamekosa nafasi ya kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United wa miaka 15 Omari Forson kwa mkataba wa kitaalamu. (Mail)
Manchester United wamehusishwa na uhamisho wa beki wa Real Valladolid na Ghana Mohammed Salisu, 21. (AS - in Spanish)
Mohammed SalisuHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Kiungo wa kati wa Leicester Wilfred Ndidi amesema anafurahia sana uwepo wake katika klabu hiyo, licha ya tetesi zinazomhusisha Mnigeria huyo wa miaka, 23, na uhamisho wa Manchester United ama Arsenal. (Teamtalk)
Kiungo wa kati wa Uhispania Dani Ceballos, 23, amesema ana matumaini ya kurejea Real Madrid mkataba wake wa Mkopo wa msimu mzima Arsenal utakapomalizika. (Movistar - in Spanish)
Mshambuliaji wa Atletico Madrid Diego Costa amesema mkufunzi wake wa zamani wa Chelsea Antonio Conte huenda "asidumu" msimu mzima katika klabu kama Real Madrid. Conte amekuwa mkufunzi wa Inter Milan tangu Mei 2019. (ESPN)
Diego CostaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mkufunzi wa zamani wa Tottenham na Chelsea Andre Villas-Boas amesema hatarudi tena katika Ligi ya Premier. (Mail)
Mshambuliaji wa Tottenham Son Heung-min huenda akakosa mazoezi ya Ligi ya Primia. Raia huyo wa Korea Kusini, 27, ambaye yuko nyumbani kwa huduma ya kitaifa atalazimika kujitenga atakaporudi. (Evening Standard)

Post a Comment

0 Comments