Tetesi za soka Ulaya Jumapili 26.04.2020 :Aubameyang, Pogba, Sancho, Neymar, Mbappe

Paris St-Germain imetoa ofa kwa kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 27, wao wakimtoa kiungo wa kati wa Argentina, 32, Angel di Maria - ambaye alishindwa kufanya vizuri akiwa Old Trafford, 2015 kama sehemu ya makubaliano. (Mail)
Baba yake mchezaji Pierre-Emerick Aubameyang, Pierre-Francois amemsihi kijana wake mshambulizi wa Gabon, 30, kusaini mkataba mpya na Arsenal kupitia akaunti ya Instagram ya mtoto wake kuhusu kusaini mkataba wake wa kwanza na klabu hiyo. (Mirror)
Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 35, ameahidi kusalia Juventus hadi 2022 wakati kuna uvumi unaomhusisha na kurejea kwa klabu yake ya zamani Manchester United. (Sun)
Borussia Dortmund inaamini kwamba inaweza kumshawishi winga wa Uingereza Jadon Sancho, 20, kusalia kwenye klabu hiyo licha ya uvumi kuwa makubaliano ya mchezaji huyo kuhamia Manchester United yameshafikiwa. (Teamtalk)
Pierre-Emerick AubameyangHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPierre-Emerick Aubameyang
Rais wa Real Madrid Florentino Perez bado ana ndoto ya kufikia makubaliano ya kumsaini mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, kulingana na ajenti wa mchezaji huyo wa Brazil, 28. (Goal)
Ni afadhali timu ya PSG ikamwacha mchezaji Kylian Mbappe kuozea kwenye benchi" badala ya kumuuza mshambuliaji huyo, 21, kwa Real Madrid. (Sun)
Kocha wa Tottenham Jose Mourinho amepigia simu moja kwa moja mchezaji wa PSG raia wa Ubelgiji Thomas Meunier, 28, katika hatua ya kutafuta mshambuliaji msimu huu. (Express)
Jadon SanchoHaki miliki ya pichaEPA
Image captionJadon Sancho
Kiungo wa kati wa Leicester City James Maddison, 23, amemuarifu shabiki wake kwamba atasalia kwenye klabu hiyo kinyume na tetesi kuwa huenda akahamia Manchester United. (Goal)
Leicester bado ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Lille Victory Osimhen, 21, lakini huenda nafasi hiyo ikashuka nchini Italia ambapo Juventus na Inter Milan wanaendeleza dhamira sawa na hiyo ya kutaka kumsajili mchezaji huyo wa Nigerian. (Mail)
Arsenal itahitajika kufuzu kwa ligi ya Champions msimu ujao ili iweze kumchukua kiungo wa kati wa Atletico Madrid raia wa Ghana Thomas Partey, 26. (Express)
Norwich imefikia makubaliano ya kumsaini mshambuliaji wa Luxembourg Danel Sinani, 23, kutoka F91 Dudelange katika makubalia ya miaka 3. (Sky Sports)

Post a Comment

0 Comments