Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 27.04.2020: Coutinho, Aubameyang, De Gea, Rakitic, Neymar

Kiungo wa kati wa Barcelona Philippe Coutinho, ambaye yuko kwa mkopo Bayern Munich, aliambiwa na Liverpool kuwa hawana mpango wa kumsajili tena mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil wa miaka 27- walipokuwa wanajadili uwezekano wake kurejea katika klabu hiyo. (Mirror)
Arsenal wamejiondoa katika mazungumzo ya mkataba wa mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang. Kiungo huyo wa kimataifa wa Gabon mwenye umri wa miaka 30-anatarajiwa kuondoka katika uwanja wa Emirates, huku klabu za Manchester United, Inter Milan, Barcelona, Real Madrid na Chelsea zikitaka kumsaini. (Mirror)
Kipa wa Manchester United, Mhispania David de Gea,29, amesema kuwa anataka kusalia Old Trafford kwa "miaka mingi" lakini nafasi yake inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Muingereza Dean Henderson, 23, ambaye ameonesha umahiri wake baada ya kusajili kwa mkopo kutoka Sheffield United. (Mail)
Pierre-Emerick AubameyangHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Ajenti wa zamani wa Neymar, Wagner Ribiero amesema mshambuliaji huyo wa Brazil na Paris St-Germain, 28, alitaka kujiunga na Chelsea alipokuwa na miaka 17. (Mail)
Beki wa Paris St-Germain na Ubelgiji Thomas Meunier "ameshawishiwa" na mkufunzi wa Tottenham Jose Mourinho kuhusu uhamisho wa msimu wa joto, lakini kiungo huyo wa miaka 28- huenda akapewa mkataba mpya Parc des Princes. (L'Equipe, via Teamtalk)
Beki wa Paris St-Germain na Ubelgiji Thomas MeunierHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBeki wa Paris St-Germain na Ubelgiji Thomas Meunier
Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard amezungumza na mshambuliaji wa Napoli Dries Mertens na anatarajia kumpata kiungo huyo wa Ubelgiji wa miaka 32, kwa uhamisho wa bure. (Mail)
Beki wa Uholanzi Jetro Willems, 26, amedokeza kuwa anataka kuhamia Newcastle kwa mkataba wa kudumu baada ya kuchezea klabu hiyo mwanzo wa msimu kutoka Eintracht Frankfurt kabla ya kujeruhiwa. (Goal)
Chelsea watamkosa kipa wa Ajax Andre Onana kwasababu mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon anajiandaa kurejea Barcelona. (Express)
Chelsea watamkosa kipa wa Ajax Andre Onana kwasababu mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon anajiandaa kurejea Barcelona. (Express)

Post a Comment

0 Comments