tangazo

Virusi vya corona: Je unaweza kuambukizwa Covid-19 kutoka kwa miili ya wafu ?

Kote duniani Covid-19 imetuacha tukishuhudia picha za vifo vya wagonjwa ambao hawana wapendwa wao wa kuwaomboleza.
Picha zote hizo zimesababisha uoga mkubwa si kutokana na kifo chenyewe, bali pia kwa wanaokufa kutokana na virusi hivyo. Uoga wa ugonjwa unasambaa kabla hata ya vifo na hata uwezekano wa kupata virusi kutoka kwa miili iliyopata maambukizi ya virusi vya corona.
Je mwili wa marehemu unaweza kuambukiz Covid-19? Je ni salama kufanya mazishi? Na je mhanga anapaswa kuzikwa au kuchomwa?
Haya ndiyo tunayofahamu:
Je miili ya wafu inaweza kueneza Covid-19?
Men carrying a coffin of a suspected Covid-19 victimHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionShirika la ASfya duniani -WHO linasema watu wanaobeba jeneza wanapaswa kuvaa mavazi ya kinga na wanapaswa kunawa mikono yao
Kwa mujibu wa Shirika la afya duniani (WHO), iwapo tahadhari muhimu zitachukuliwa , hakunasababu ya kuogopa kusambazwa kwa Covid-19 kupitia miili ya wafu.
Virusi vya Sars-CoV-2 , ambavyo ndivyo vinavyosababisha ugonjwa, huenezwa zaidi kwa njia ya cheche za mate au ute unaotoka kwa binadamu, kwa mfano wakati tunapozungumza kupiga chafya au kukohoa.
Hatahivyo , vinaweza kuishi kwa hadi siku kadhaa kwenye vitu fulani vigumu.
"Hadi leo , hakuna ushahidi kuhusu hali ya maambukizi kutoka kwenye ya binadamu iliyokufa kwa binadamu hai ," alisema William Adu-Krow, msemaji wa Shirika la afya la Marekani -Pan-American Health Organization (PAHO/ WHO), wakati wa mkutano na waandishi wa habari mapema mwezi huu.
Je virusi vinaweza kuishi katika miili iliyokufa?
A relative mourns the death of a man with Covid-19 in the Iraqi city of Najaf, March 2020Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMiili iliyokufa inaweza kuhifadhi virusi katika viungo vya mwili kwa hiyo tahadhari zinahitajika wakati wa kuishughulikia miili ya wafu
"Kwa kusema hivyo, haimaanishi kwamba kwasababu tunasema haiwezi kuambukiza, na unampenda mpendwa wako aliyekufa na corona sana kwa hiyo unaweza kumbusu au kufanya chochcote cha aina hiyo ," aliongeza mtaalamu huyo.
"Bado tutatakiwa kuzingatia ushauri wa kuzuwia na kudhibiti maambukizi ."
Maagizo ya WHO yaliyotolewa mwezi Machi yalisema kwamba "isipokua watu waliokufa kwa magonjwa kama Ebola, Marburg na kuhara, miili ya wafu kwa ujumla huwa haina maambukizi
"Ni mapafu tu ya wagonjwa wenye mlipuko wa ambayo yasiposhughulikiwa kwa uangalifu wakati wa uchunguzi yanayoweza kusababisha maambukizi. Vinginevyo, kiwiliwili cha mfu hakiwezi kusambaza maambukizi ."
Lakini maiti za watu waliokufa kutokana na ugonjwa mbaya wa mfumo wa kupumua inaweza kuwa na virusi hai katika mapafu yao na viungo vingine vya miili yao.
Virusi hivi vinaweza kutolewa wakati wa upasuaji wa uchunguzi wa mwili, ambapo vifaa vya kimatibabu hutumiwa, au wakati wa kuosha ndani ya mwili.
Ndugu na marafiki wa mhanga wa Covid-19 wanapaswa kuhakikisha mwili unaandaliwa kwa mazishi au kuuchoma na mtu ambaye amepata mafunzo yanayofaa na wataalamu waliojikinga kwa mfana watoaji wa huduma za mazishi.
Je mazishi yanaweza kufanyika?
Mazishi yamepigwa marufuku au kuwa na masharti makali kote duniani kutokana na Covid-19Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMazishi yamepigwa marufuku au kuwa na masharti makali kote duniani kutokana na Covid-19
Katika baadhi ya maeneo kuongezeka kwa idadi ya kubwa ya vifo vinavyotokana na Covid-19- kumesababisha kuwepo kwa mzozo katika sekta ya mazishi.
Na kufuata kanuni za kutosogeleana katika jamii, mazishi yamepigwa marufuku katika nchi kadhaa.Baadhi bado zinaruhusu mazishi, lakini yanayohudhuriwa na idadi ndogo sana ya watu.
WHO inasema wanafamilia na marafiki wa marehemu wanaweza kutazama mwili wakati wa mazishi, ilimradi wazingatie masharti fulani yaliyowekwa.
"Hawapaswi kugusa au kubusu mwili na wanapaswa kunawa mikono yao vema kwa sabuni na maji baada ya kuutazama mwili, hatua za kukaa mbali na mwili zinapaswa kuzingatiwa (walau kuwe na umbali wa mita moja baina ya watu )," muongozo wa WHO unasema.
Watu wenye dalili za magonjwa ya mfumo wa kupumua hawapaswi kuhudhuria mazishi au iwapo watalazimika wanapaswa kuvaa barakoa kuzuwia kusambaa kwa maambukizi, uliongeza
Na watoto, watu wazima wenye umri wa zaidi ya miaka 60 na wenye kinga dhaifu ya mwili hawapaswi kabisa kuukaribia mwili.
Je miili inaweza kuzikwa, au inapaswa kuchomwa ?
Aerial view of new graves in the Brazilian city of Manaus, hard-hit by the Covid-19 pandemicHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPicha ya makaburi mapya katika jiji la Brazil la Manaus; miji mingi imekumbwa na vidadi kubwa ya vifo vinavyosbabishwa na virusi vya corona
WHO inasema kumzika na kumchoma mfu aliyekufa kutokana na corona youte inakubalika
" Ni imani ya kawaida kwamba watu ambao wamekufa kutokana na magonjwa yanayoambukuza wanapaswa kuchomwa, lakini hilo si kweli. Kuchoma maiti ni suala la utamaduni unaochaguliwa na hii si kweli. Kuchoma mwili ni sula la utamaduni wa kuchagua na raslimali zilizopo," uliongeza.
Wale wanaoshughulikia miili- kwa mfano , kuiweka kaburini, wanapaswa kuvaa glove na kunawa mikono yao vyema kabla na baada ya kutupa glove.
Hakuna haja ya kuzika miili ya wahanga wa Covid-19 haraka, iliongeza WHO.
Sio lazima kuharibu au kuchoma vifaa alivyotumia muhanga wa corona aliyekufa, lakini vinapaswa kushughulikiwa na mtu aliyevalia glove na kuwekwa katika kemikali za kuua vimelea vyema, mfamo katika kemikali zenye 70% ya mchambnganyiko wa kemikali ya ethanol au blichi.
Nguo zinaweza kufuliwa kwa kemikali za kufua nguo kwa joto (nyuzi joto 60−90°C) au ziwekwe ndani ya maji ya moto na sabuni katika pipa kubwa, na zigeuzwe kwa fimbo na epuka kumwagikiwa na maji yanayotoka katika pipa lenye nguo hizo.

Hadhi ya mtu ilindwe

Katika jiji la Ecuadorian la Guayaquil, miili ya wafu iliachwa mitaani wakati hifadhi ya maiti ilipajaaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKatika Jiji la Ecuadorian la Guayaquil, miili ya wafu iliachwa mitaani wakati hifadhi ya maiti ilipajaa
WHO inasema kwamba "hadhi ya mfu, tamaduni zao na uamaduni zao za kidini, pamoja na familia zao vinapaswa kuheshimiwa na kulindwa wakati wote ".
Lakini huku mkanganyiko ukisambaa, hili limemeonekana kuwa jambo gumu sana katika baadhi ya maeneo ya dunia.
Merwin Terán, mkuu wa muungano wa wafanyabiashara za huduma za mazishi, aliiambia BBC kuwa hali "imekua si hali" katika ijimbo la Guayas, ambako vifo vya where Covid-19 d vimepita 10,000 katika kipindi cha wiki kadhaa
Ecuador ni nchi ya pili iliyoathiriwa zaidi na korona katika bara la Amerika Kusini, nyuma ya Brazil. Mifumo ya afya imeshindwa kuhimili shinikizo la ugonjwa, majeneza na miili ya watu waliokufa imekua iliachwa kwa siku kadhaa kwenye mitaa kutokana na kufurika kwa hifadhi za maiti.
Hospitali zimekua zikipeleka miili ya watu katika karakana ambazo hazina viyoyozi na miundombinu inayofaa katika kuhifadhi maiti.
"Hata sisi, ambao tumezowea kushuhudia hali halisi ya kifo , ni vigumu kuingia katika karakana kutambua mwili. Maiti zilikua zinapasuka na kutoa vimiminika baada ya saa 24 ," anasema Terán.
Wahanga wanaoshukiwa kuwa ni wa Covid-19 wakizikwa Insanbul Uturuki. WHO inasematunapaswa bado kuwaheshimu wafuHaki miliki ya pichaEPA
Image captionWahanga wanaoshukiwa kuwa ni wa Covid-19 wakizikwa Insanbul Uturuki. WHO inasematunapaswa bado kuwaheshimu wafu
Kwingineko , picha za makaburi ya watu wengi mjini New York, katika jiji la Brazili la Manaus au Istanbul ziligonga vichwa vya habari.
Lakini ukweli ni kwamba ukatili wa kifo cha virusi vya cororona haupaswi kusababisha watu waliokufa kwa corona kutoiagwa kwa hadhi ya utu walionao, inasema WHO -na kuwaruhusu wapendwa wao kuwa na fursa ya kuomboleza.
"Maafisa wanapaswa kushughulikia ipasavyo kila hali kulingana na kwa misingi ya utofauti wa kisa na kisa cha corona, kutathmini uwiano wa haki za familia ya marehemu , haja ya kuchunguza sababu ya kifo, na hatari ya kusambaza maambukizi ," linasema shirika hilo

Post a Comment

0 Comments