tangazo

Virusi vya corona: Mama apikia watoto wake mawe kwasababu ya kukosa vibarua alivyokuwa akifanya awali

Mjane mmoja nchini Kenya amepikia watoto wake mawe kuwadanganya kwamba chakula kinaiva.
Mwanamke mmoja nchini kenya ameelezea vile ambavyo amekuwa akiwapikia watoto wake mawe kuwadanganya kwamba chakula kinaiva.
Penina Bahati, mama wa watoto wanane hajafanikiwa kupata kazi zisizohitaji ujzi ambazo amekuwa akifanya siku za nyumba kutafutia watoto wake chakula cha kila siku.
Mjane huyo anayeishi maeneo ya pwani mji wa Mombasa anaweka mawe na maji sufuriana na kuyaweka motoni hadi watoto wake watakapo lala.
NjaaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Kituo cha Runinga cha NTV kiliweka video mtandaoni inayomuonesha mama huyo akipika mawe hayo.
Jirani yake aliamua kuelezea kituo hicho cha habari masaibu yake baada ya kumshuhudia akipika mawe alipokwa amekwenda nyumbai kwake na kuanza kutoa wito kwenye mitandao ya kijamii isaidie kumpa mama huyo msaada wa chakula.
Mama huyo anayefahamika kama Bahati, amekuwa akipokea pesa kupitia simu ya mkononi pamoja na kufunguliwa akaunti na jirani yake ili aweze kupata usaidizi.

Post a Comment

0 Comments