tangazo

Virusi vya corona: Nadharia za uongo kuhusu virusi vya corona kati ya Marekani na China

Kuanzia siku za mwanzo za mlipuko wa virusi vya corona, nadharia zisizo za kweli kuhusu chimbuko na ukubwa wa janga la corona ni miongoni mwa yaliyoenea kwenye mitandao.
Hilo halikusaza madai ya uongo kwamba virusi vya corona ilikuwa sehemu ya mpango wa China ya "kuficha mpango wake wa 'silaha za kibaiolojia", na madai yasio na msingi wowote kwamba timu ya kijasusi ya Canada ambayo chimbuko lake ni China ilituma virusi vya corona hadi mji wa Wuhan.
Madai ya kwamba virusi hivyo vimetengenezwa na mwanadamu yamevumishwa na makundi yakihasidi yenye njama fulani kwenye mitandao ya Facebook, kwenye akaunti za Twitter zisizokuwa sahihi na hata kujipenyeza hadi katika Televisheni ya Taifa ya Urusi inayomilikiwa na serikali wakati wa taarifa kuu.
Na miezi kadhaa baada ya mlipuko huo, sio tu kwamba kufuta nadharia hizo imekuwa kibarua kigumu lakini pia madai mengine mapya yameibuka na kunadiwa na maafisa wa serikali, wanasiasa waandamizi na vyombo vya habari vya China na Marekani.
'Madai ya uzushi'
Zhao Lijian, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, alisemekana kusema kuwa - bila hata Ushahidi kwamba ugonjwa wa Covid 19 huenda ikawa chanzo chake ni Marekani.
Machi 12, kupitia mtandao wa Twitter, aliandika kwamba kuna uwezekano mkubwa jeshi la Marekani liliingiza virusi hivyo mjini Wuhan.
Siku moja baadae, alituma kwenye mtandao wa Twitter, makala ya tovuti ya Global Research yenye kichwa "Ushahidi zaidi kuwa chimbuko la virusi vya corona ni Marekani", na kusihi wasomaji wasome makala hiyo na kushirikisha wengine. Hatahivyo, makala hiyo kwasasa imefutwa kwenye mtandao wa Twitter.
Gazeti la kila siku la China la The Global Times liliunga mkono taarifa za Bwana Zhao. Na kusisitizia kwamba mwanadiplomasia huyo amesema madai hayo kama mtu kibinafsi, matamshi yaliyoendana na mashaka yaliyoonyeshwa na raia wa China", gazeti hilo liliandika.
Madai ya Bwana Zhao yamekuwa yakiboreshwa na kutolewa na balozi kadhaa za China na watumiaji wa mitandao ya kijamii katika sehemu mbalimbali duniani duniani.
Mtaalamu wa China wa kitengo cha BBC Monitoring Kerry Allen, amesema kwamba Bwana Zhao anafahamika kwa kuwa mzungumzaji mzuri - hasa kwenye mitandao ya kijamii - ni mtu mwenye mtazamo tofauti ndani ya China bara na sio kwamba kila anachozungumza huwa ni kwa niaba ya uongozi.
Taasisi iliyoanzishwa 2001 huko Canada ya Global Research, ni tovuti ya kituo cha Utafiti kuhusu utandawazi. Kulingana na tovuti inayoangalia usahihi wa madai yaliyoibuliwa, kituo kinachojitegemea cha Marekani, " Global Research imekuwa na nadharia za uwongo kuhusu masuala kama vile 9/11, chanjo na mabadiliko ya tabia nchi.
Lakini utafiti wa China na makala katika majarida ya kisayansi aliokuwa ananukuu hata hayatoe wito wa kuhoji China, chimbuko la mlipuko. Badala yake, yanaangazia soko la wanyama pori mjini Wuhan huenda sio kiini cha ugonjwa wa virusi vya corona.
Bwana Romanoff pia anadai kwamba wanasayansi wa Japani na Taiwan "Wameonesha kuwa virusi vipya vya corona huenda chimbuko lake ni Marekani".
Lakini hitimisho linaonekana kuzingatia kile ambacho ni taarifa za kwenye televisheni moja ya Japani iliyotolewa mwezi wa Februari, pamoja na madai yaliyotolewa na televisheni moja ya Taiwan na mtaalamu wa dawa profesa mmoja ambaye sasa ni mwanasiasa wa chama tawala cha China ambaye Bwana Romanoff anaanza kwa kumtambulisha kimakosa eti yeye ni mtaalamu wa virusi jambo ambalo sio ukweli.
Bwana Romanoff pia anadai kwamba - bila ushahidi - maabara ya kijeshi ya Marekani ya kuchunguza viini huko Fort Detrick, Maryland, huenda ikawa ndo chanzo cha virusi hivyo. Aliongeza kuwa halitokuwa jambo la kushangaza kwasababu kituo hicho kilifungwa kabisa mwaka jana kwasababu ya ukosefu wa ulinzi wa kuzuia viini kuvuja.
Kulingana na vile gazeti la New York Times lilivyoandika, sio kwamba kituo hicho kilifungwa kabisa, lakini kiliahirisha shughuli zake za utafiti na msemaji akatoa hakikisho kwamba hakuna nyenzo zozote hatari zilizotoka nje ya maabara hiyo.
'Nchini China'
Bwana Romanoff anajitambulisha kama mshauri aliyestaafu na mfanyabiashara, na profesa wa muda wa Chuo Kikuu cha Fudan kilichopo Shanghai.
BBC News imezungumza na Chuo Kikuu cha Fudan kuthibitisha ikiwa Bwana Romanoff anajihusisha na chuo hicho kama profesa wa muda lakini haikupata jibu lolote.
Mchangiaji wa mara kwa mara wa Global Research, ambaye makala zake nyingi zinaonekana kukosoa Marekani na kuunga mkono China, ikiwemo makala aliyoelezea maandamano katika uwanja wa 1989 iliyofahamika kama "American-instigated colour revolution".
Miongoni mwa madai mengine mengi, katika chombo cha habari mwezi jana, alisema katika nyakati za awali za ugonjwa wa Covid-19 kuwa ulikuwa ni wa "China" na wala ugonjwa huo haukuwa na uwezo wa kuathiri watu wa asili nynegine.
BBC News ilijitahidi kuwasiliana na Bwana Romanoff lakini hakujibu lolote.
'Virusi vya Corona vilivuja kwa bahati mbaya kutoka kwenye maabara'
Madai ya serikali ya China na vyombo vya habari kuwa Marekani huenda ikawa ndo kitovu cha virusi hivyo yalifanya Rais Trump kuzungumza, ambaye alirejelelea ugonjwa wa Covid-19 kama virusi vya China. Na Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo alitaka China iache kusambaza taarifa za uwongo.
Hivi karibuni, Rais Trump alitangaza kwamba atasitisha ufadhili kwa Shirika la Afya Duniani (WHO), na kulishtumu kwa kupendelea China.
Kama jibizo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema huu si wakati wa kusitisha ufadhili kwa shirika hilo la Umoja wa Mataifa.
Lakini wanasiasa kadhaa Marekani na wachambuzi pia wamekuwa wakivumisha madai kadhaa kuhusu chimbuko la virusi hivyo.
Taafiri ya habari ya Fox News iliyosomwa na Tucker Carlson akiongeza uwezekano wa kwamba virusi vya corona kwa bahati mbaya vilikwepa kutoka kwa maabara ya mji mmoja wa Wuhan.
Na maseneta wa chama cha Republican Tom Cotton na Ted Cruz, pia nao wamewahi kuzungumzia madai kama hayo.
Utafiti uliochapishwa awali Februari kama rasimu ya ripoti yenyewe ilikuwa ni ya watafiti wawili wa China - Botao Xiao na Lei Xiao kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Guangzhou Kusini mwa China - na wala haukuwa umepitiwa. Ulihitimisha kwamba virusi vya corona pengine huenda chimbuko lake ni Wuhan.

Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionPresident Trump has accused the WHO of being "China-centric"
Tangu wakati huo, Bwana Xiao amekuwa akiliambia Jarida la Wall Street kwamba alifuta utafiti huo. Wasiwasi kuhusu kiini cha virusi vya corona, kulizingatia makala za kitaaluma na vyombo vya habari wala hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja," kulingana na jarida la Wall Street Journal lililomnukuu.
Gazeti la Washington liliripoti katikati ya Aprili kwamba wanadiplomasia wa kisayansi wawili kutoka ubalozi wa Marekani walitembelea Taasisi ya Virusi ya Wuhan mwaka 2018 na kuonya Washington kuhusu "ukosefu wa usalama kwenye maabara, ambayo ilikuwa inafanya utafiti kuhusu hatari ya virusi vya corona kutoka kwa popo".
Jeremy Konyndyk, aliyeongoza seriakali ya Marekani wakati wa kupambana na mlipuko wa Ebola, pia aliwahi kutuma ujumbe kwenye Twitter kuhusu taarifa ya kuvuja kwa virusi kwenye maabara.


Post a Comment

0 Comments