Virusi vya corona : Namna nchi za Afrika zinavyotekeleza amri ya kutotoka nje

Nchi za Afrika zina watu wachache walioathirika na virusi vya corona kuliko nchi nyingine duniani, lakini mifumo duni ya kiafya inafanya bara la Afrika kuwa katika hatari.
Katazo la kutotoka nje linaweza kuzuia kuenea kwa virusi, lakini serikali zimechukua mikondo mingine ya kuweka makatazo kwa raia.

Kuna nchi ambazo zimeondoa masharti?

Baadhi, kama Ghana kwa sasa zinapunguza makali ya hatua hizi, hasa wakizingatia athari kwa watu masikini na kwasababu pia wamechukua hatua nyingine dhidi ya virusi hivi.
Ghana iliweka marufuku kutoka nje katika miji yake mikubwa- ambayo kwa sasa marufuku hizo zimeondoshwa. Lakini kuzuiwa kwa shughuli za kijamii, na shule zitaendelea kufungwa kwa sasa.
''Marufuku ilikuwa inaanza kuwa na athari mbaya kwa masikini hasa wale wanaotegemea mauzo ya kila siku ili kujikimu kimaiasha,'' anasema mwandishi wa BBC Thomas Naadi.
Rais wa Ghana Nana Akufo-Ado amesema ongezeko la kasi ya upimaji na kuboreshwa kwa vituo vya tiba kulimaanisha kuwa hatua zinaweza kulegezwa.
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo pia imepunguza baadhi ya makatazo katika baadhi ya maeneo ya mji mkuu wake Kinshasa, ambayo aliathiriwa sana na virusi vya corona.
Na nchi nyingine hazikuweka masharti makali tangu awali.
Tanzania iliripoti mgonjwa wa kwanza na serikali ilifunga taasisi za elimu, lakini mikutano ya kidini haikupigwa marufuku, isipokuwa kusitisha kwa safari kimataifa tarehe 11 mwezi Aprili.
Lakini suala hili linaweza kuwa na athari mbaya, kwa mujibu wa Shirika la Afyaa duniani, WHO.
''Tumeona kuwa kutochangamana, ikiwemo kuzuiwa kwa mikusanyiko , kumechukua muda mrefu kutekeleza,'' anasema Matshidiso Moeti wa WHO.
Ameongeza kuwa kuchelewa huku ni sababu ya kuwepo kwa ongezeko kubwa la maambukizi.
Vizuizi Afrika KusiniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionVizuizi Afrika Kusini
Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dokta Tedros Ghebreyesus amesema nchi zinapaswa kuhakikisha kuwa uwezo wa kugundua, kupima,kutenga na kuwatunza watu waliothibitishwa kuwa na maambukizi wakati wakilegeza marufuku hizo.
''Kuondoa marufuku ya kutotoka nje haimaanishi kuwa ni mwisho wa ugonjwa huo katika nchi yoyote, ni mwanzo tu wa awamu ya pili,'' aliongeza.

Nani ameweka sheria kali?

Nchi nyingi za Afrika zimekuwa katika mapambano dhidi ya magonjwa ya kuambukiza, nyingi zilichukua hatua kali hata kabla ya kuripotiwa kwa milipuko.
Nchi 13 zilifunga shule kabla ya kuripotiwa kwa wagonjwa wa kwanza wa Covid-19.
Serikali ya Afrika Kusini imesema itapunguza makali ya marufuku ya kutotoka nje kuanzia tarehe 30 mwezi Aprili, lakini kwa sasa inatekeleza moja kati ya hatua kali za kutotoka nje kuliko pengine popote duniani.
Imefunga shule, vyuo, na kumekuwa na idadi ndogo ya watu wanaotembelea wagonjwa hospitalini na magerezani. Mikusanyiko ya Umma, isipokuwa mazishi imepigwa marufuku- na jeshi linafanya kazi mitaani kuhakikisha amri hiyo inatekelezwa.
Afrika Kusini inatekeleza hatua kali barani AfrikaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAfrika Kusini inatekeleza hatua kali barani Afrika
Nigeria taifa lililo na watu wengi Afrika, lilifunga mipaka yake na kuzuia safari za ndege za kimataifa mwishoni mwa mwezi Machi.
Kisha ikafunga miji yake mikubwa Lagos na Abuja baada ya zaidi ya watu 100 kuthibitishwa kuwa na maambukizi, kisha wakazuia safari za jimbo moja kwenda jingine.
Zimbabwe ilichukua hatua wakati huohuo pia, ingawa ilikuwa na idadi ndogo ya walioambukizwa.
Kenya iliweka amri ya kutotoka nje kwa baadhi ya maeneo, huku safari za kuingia na kutoka nje ya miji mikubwa ikizuiwa. Pia ilikuwa na muda wa mwisho wa kuwa nje, watu 400 walikamatwa kwa kukiuka amri hizo.

Je marufuku ya kutotoka nje ni mwafaka kwa nchi za Afrika?

Kituo cha kupambana a kudhibiti magonjwa barani Afrika kimeiambia BBC kuwa marufuku ya kutotoka nje imesaidia kupunguza maambukizi mapya.
''Bila marufuku hii kungekuwa na mlipuko mkubwa zaidi,'' anasema Mkurugenzi wa kituo hicho John Nkengasong.
Maabara ya KenyaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMaabara ya Kenya
Aliongeza kuwa si marufuku hiyo pekee, bali pia kile unachokifanya wakati wa marufuku hiyo.
''Unaongeza kasi ya upimaji, kuwatenga walioambukizwa na kuwatafuta watu waliochangamana nao ili ukiondoa marufuku hiyo unakuwa umetengeneza matokeo mazuri katika mapambano dhidi ya kusambaa kwa virusi vya corona.''
Ni muhimu kusema kuwa virusi vya corona ni hatari kwa watu walio na umri mkubwa, mfano ilivyosabaisha athari kwa nchi za Ulaya.
Watu wa umri wa wastani wa kati nchini Italia na Marekani kama 45 na 40 kwa mfano, ambapo ni wastani wa karibu miaka 20 kwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.
Hatahivyo, haina maana kuwa hakuna sababu nyingine, kama usafi na kukosekana kwa huduma nzuri za kiafya.
Baadhi ya watu wamehoji kuhusu hitaji la kuendelea na marufuku ya kutotoka nje, kwa mfano chama tawala Afrika Kusini.
Kumekuwa na masuala ya athari za kiuchumi- Nchi za Magharibi wametenga fedha nyingi ili kusaidia biashara na mifumo ya ustawi wa jamii. Lakini nchi za Afrika hazina uwezo huo.
Kuna masuala ya haki za binaadamu yameibuliwa kuhusu tabia za baadhi ya vikosi vya usalama wanaposimamia marufuku hizo.
Shirika la Amnesty International liliripoti matukio ya udhalilishaji unaofanywa na vikosi vya usalama Afrika Kusini, Kenya, Zimbabwe na Nigeria.
''Majimbo mengi yameongezea nguvu ya polisi na jeshi, na katika sehemu nyingi zimesababisha ongezeko la ukiukaji wa haki za binaadamu,'' anasema Eda Seyhan katika kituo cha Covid State Watch kinachotazama masuala ya ukiukaji wa haki za binaadamu wakati huu wa janga la corona.

Post a Comment

0 Comments