ACT Wazalendo yatimiza miaka sita, Zitto atoa ujumbe

Chama cha ACT WAZALENDO Nchini Tanzania leo Jumanne tarehe 5 Mei 2020 kinaadhimisha miaka sita tangu kiliposajiliwa .

''ACT WAZALENDO kilipata usajili wa kudumu tarehe 5 Mei 2014 .kilishirikiuchaguzi mkuu kwa mara ya kwanza uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu2015.

Katika uchaguzi huo , kilisimamisha wagombea ubunge kwenye maeneo mbalimbali Nchinina kufanikiwa kushinda jimbo moja la Kigoma Mjini linaloongozwa na Zitto Kabwe. Pia kilishinda nafasi ya udiwani kwenye maeneo kadhaa ikiwemo Kigoma Ujiji hali iliyokifanya kuongoza halmashauri ya Kigoma Ujiji.

Katika salamu zake alizotoa leo Jumanne kuadhimisha miaka sita ,Zitto Kabwe kiongozi wa chama hicho amesema imekuwa miaka sita ya kupigania makundimbalimbali ya watanzania bila kuchoka.

Miaka sita ya majaribu mengi katika maisha yetu ya kila siku .act wazalendo tumekuwa upande wa wananchi muda wote, wakati wote bila kujali athari zitakazotupata.

-Tumekuwa na wazanzibari walipoporwa haki yao ya kuchagua kiongoziwanaemtaka

-Tumekuwa na wakulima wa mbaazi ,korosho,pamba,tumbaku, na karafuuwalipoharibu masoko ya bidhaa zao na kudhulumiwa fedha zao zitakazotokana na jasho lao.

-Tumekuwa na wavuvi baharini na ziwani walipochomewa nyavu zao na kuharibiwa maisha yao.

-Tumekuwa na wafugaji walipovamiwa kuondolewa maeneo ya malisho ya mifugo yao.

Tumekuwa na wafanyabiashara walipobambikiwa kodi kubwa ,kutolipwa fedhazao za marejeshona kufunguliwa kesi za utakatishaji.

Tumekuwa na wanaharakati wa haki za kibinaadamu waandishi wa habari walipobambikiwa kesi na kuwekwa jela,kutekwa, kupotea na hata kuuwawa.

Tumesimamia uhuru wa taasisi ya uwajibikaji kama CAG na kuhakikisha katiba ya Tanzania inalindwa na kuheshimiwa.

Tumekuwa na wanasiasa wenzetu wanapoonewa na kunyimwa haki zao bila kujali vyama vyao.\
Tumekuwa na wananchi kuwaalimisha kujikinga na virusi vya corona ili kuzuia vifo vya watu wetu na kuiwajibisha serikali .

Kila mwenye kuonewa ,kudhulumiwa na kukandamizwa anasikia sauti ya ACT WAZALENDO bila kujali chama chake, dini yake, kabila lake wala hali yake. hakika ulio tupo

Ninawaomba muipe dhamana ACT wazalendo ili ijenge Tanzania inayopaa kiuchumi,yenye qatu wenye raha na furaha.

Post a Comment

0 Comments