tangazo

Ahukumiwa kunyongwa kwa kumuua mkewe

Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya kigoma imemuhukumu raia wa burundi , mkazi wa kijiji cha Rungwe Mpya ,Wilaya ya Kasalu Yohana Philipo ( 28) kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua kwa makusudi mke wake wa wazamani Scolastica James kwa kumchoma kisu shingoni na kufariki dunia

hukumu hio ilitolewa na jaji wa mahakama hiyo, Athmani Matuma baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha kosa hilo. amesema mahakama hio imetoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwake na kwa vijana wengine wenye tabia ya kikatili kama yeye

Wakati wako shambani Scolastica Jmaes na shamim moshi , walienda mtoni kuchota maji wakati wakiwa wamebeba ndoo zao kichwani, ghafla mshtakiwa alimvamia Scolastika na kumchoma kisu shingoni na kukosa hewa baada ya kuvuja damu nyingi na alifariki dunia.

Jaji alisema Scolastica alikufa kifo cha kikatili mbele ya macho ya shahidi namba moja ambaye alitoa ushahidi wake wa ukweli na wakuaminika maana alishuhudia mshatakiwa akimchoma kisu mke wake wa wazamani.

Post a Comment

0 Comments