tangazo

Baada ya Mama steve kuolewa Barnaba naye aanza mipango ya ndoa

Msanii wa muziki Bongo na mmiliki wa studio za High Table Sound, Barnaba ameweka wazi kuwa yupo katika mipango kumuoa mwanamke ambaye yupo naye kwa sasa.

Akizungumza jana kwenye kipindi cha Homa cha TV E, Barnaba amesema yupo katika mahusiano ambayo anayafurahia, hivyo suala la yeye kuoa lipo katika mchakato.
-
“Sijaoa bado Mwenyezi Mungu akijaalia nipo kwenye harakati za kumuoa mwanamke wangu ninaempenda na ananiangalia (She is my everything)” amesema.

Kauli hiyo ya Barnaba inakuja zikiwa ni wiki kadhaa tangu aliyekuwa mpenzi wake, #Zuu ambaye pia ni mzazi mwenza kuolewa.

Sanjali na hilo, Barnaba alipoulizwa kama amewahi kuzichapa na mume wa Mama mtoto wake, alisema, “Mimi na mchizi hatujawahi kupigana, kitu ambacho naamini hata hii ndoa ni jambo la baraka sababu Mama mtoto wangu sio adui yangu.

Aliongeza, “Nipo kwenye mahusiano yangu mengine anayaheshimu na mimi naheshimu mahusiano yake na mpenzi wake ambae ni mumewe kwa sasa. Tuliachana kwa wema haikuwa vita”.

Post a Comment

0 Comments