tangazo

Baba amjeruhi mwanae na kitu chenye ncha kali kisha naye kujichoma tumboni na utumbo wake kutoka nje

Jeshi la polisi mkoani Katavi linamshikilia Alfan Mlewa mwenye umri wa miaka ishirini na minane mkazi wa kitongoji cha Mnyagala 'A' wilaya Tanganyika kwa tuhuma za kumkata na kitu chenye ncha kali mtoto wake mwenye umri wa miaka mitatu kisha naye kujichoma tumboni na utumbo wake kutoka nje baada ya kuwaona polisi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi ACP Benjamini Kuzaga amesema tukio hilo limetokea May 8, mwaka huu majira ya saa 1:00 usiku.

Hata hivyo amesema kutokana na operesheni inayoendelea dhidi ya watuhumiwa wa mauaji na makosa mengine kikanda wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa May 9, mwaka huu.

ADVERTISEMENT

Post a Comment

0 Comments