Balozi Seif: Wawakilishi wa CCM kusambaza Barakoa katika majimbo yao hivi karibuni

Wajumbe wa Kamati ya Wawakilishi wa Chama cha Mapinduzi ya Baraza la Wawakilishi wameamua kutenga Shilingi Milioni 33,000,000/- kutoka Benk katika   Fedha za Mfuko wa Kamati hiyo zitakazotumika katika utengenezaji wa Mask zitazosambazwa katika Majimbo yao ili kuwasaidia Wananchi kujikinga dhidi ya Virusi vya Corona.


Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa Taarifa hiyo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kufuatia kumalizika kwa Kikao chao cha kawaida kilichopokea Taarifa ya Uwasilishwaji wa Mchango wao wa Shilingi Milioni 50,000,000/-  zilizotolewa kuunga mkono nguvu za Serikali katika mapambano dhidi ya Corona.

Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar amepokea msaada wa vifaa mbali mbali vilivyotolewa na Mfanyabiashara Mzalendo Nchini Mohamed Ibrahim Raza { Raza Lee}kwa ajili ya kusaidia nguvu za Serikali za kupambana na Corona.

Akikabidhi msaada huo wa vifaa Mfanyabiashara Mohamed Ibrahim Raza {Raza Lee} amemuahidi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba yuko tayari wakati wowote kutoa mchango wake pale itakapohitajika kufanya hivyo.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipokea mchango wa  Tani 12 wenye Thamani ya Shilingi Milioni 21,000,000/- za Vyakula mbali mbali vilivyotolewa kwa pamoja kati ya Uongozi wa Taasisi ya Misaada ya Direct Aid  kwa kushirikiana na Manispaa ya Jiji la Zanzibar.


Wakitoa taarifa ya mchango huo Meya wa Jiji la Zanzibar Mstahiki Saleh Juma Kinana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Misaada ya Direct Aid Dr. Ayman Mohamed Jamal kwa pamoja walisema msaada huo ni muendelezo wa Ushirikiano uliopo kati ya Taasisi hizo na Serikali Kuu.

Post a Comment

0 Comments