tangazo

Kwa nini Trump na Obama wameanza malumbano mapya kuhusu Flynn?

Uamuzi wa kushangaza wa Idara ya haki nchini Marekani kuondoa mashtaka yote dhidi ya alikyekuwa mshauri wa kiusalama wa rais Donald Trump , umezua shutuma chungu nzima.
Na wahusika walio katikati ya shutuma hizo ni rais wa zamani na yule wa sasa.
Michael Flynn alilazimishwa kujiuzulu mapema wakati wa kuanza kwa utawala wa rais Trump kwa kumdanganya makamu wa rais Mike Pence kuhusu mawasiliano yake na maafisa wa serikali ya Urusi.
Pia alikiri kuwadanganya maajenti wa FBI waliokuwa wakichunguza uhusiano wa Urusi na kampeni ya rais Donald Trump.
Baada ya miaka kadhaa ya migogoro, jenerali huyo wa zamani ni mtu aliyewachiliwa huru.

Je Trump na Obama wanasema nini?

Obama amezuia mdomo wake kwa muda mrefu kuhusu vitendo vya mrithi wake lakini siku ya ijumaa , katika mkutano na washauri wake 3000 na maafisa uliovuja , aliamua kuzungumza.


ADVERTISEMENT
''Hakuna mfano unaowachwa na mtu ambaye alishtakiwa kwa kudanganya na kuwachiliwa huru'', alisema.
''Haya ndio mambo ambayo yanakufanya kuwa na wasiwasi - sio tu maadili yetu - lakini uelewa wetu na sheria zinazotuongoza zipo hatarini'''.
Trump ambaye hajawahi kuogopa kushutumu ama kumlaumu mtangulizi wake , alijibu kupitia machapisho chungu nzima siku ya Jumapili, akimshutumu Obama na washauri wake kuanzisha juhudi za kihalifu kuhujumu uongozi wake.

Trump na ObamaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Alimshutumu Obama na aliyekuwa naibu mkurugenzi wa shirika la FBI Andrew McCabe , aliyekuwa naibu mwanasheria mkuu Rod Rosenstein , mtangazaji wa runinga Jimmy Kimmel na waandishi kadhaa pamoja na vyombo vya habari.
Uhalifu mkuu wa kisiasa katika historia ya Marekani , rais aliandika akijibu chapisho la mtangazi mmoja wa redio ambaye aliwashutumu maafisa wa Obama kwa kumuhujumu Trump siku chache kabla ya kuchukua uongozi.

Kwa nini kuna mgogoro?

Rais Trump mara kwa mara alitumia neno Obamagate - akifananisha kashfa ya rais Nixon ya Watergate - kuhusiana na madai yake huku wanaharakati wa kihafidhina na makundi yanayomuunga Trump yakitumia neno hilo katika alama zao za reli.
Ijapokuwa neno hilo lilitumika na Trump mapema, siku ya Jumapili lilitumika mara milioni 2 katika mtandao wa twitter- ikiwa ni ushahidi wa uwezo wa Trump alionao katika mtandao.
Umaarufu wake ulianza mapema siku ya Jumapili nchini Marekani na asilimia 86 ulikuwa kupitia retweets , ikimaanisha kwamba kulikuwa na ushirikiano fulani.
Lakini hakuna ushahidi kwamba kulikuwa na wahalfu wa mitandaoni waliotumika.

Kwa nini mashtaka hayo yalifutiliwa mbali?

Uamuzi wa kufutilia mbali mashtaka hayo ya kusema uongo dhidi ya Flynn ulifanywa na wakili wa serikali ambaye mwanasheria mkuu Bill Barr alimuajiri ili kuchunguza mashtaka.
''Kwa sababu ya uchunguzi wa FBI kuhusu kandarasi ya Flynn na uhusiano wake na maafisa wa Urusi mashtaka hayo hayakuwa na umuhimu katika kiwango hicho'', Barr alisema,
''Flynn hakufaa kushtakiwa kwa kusema uongo kuhusu suala hilo''.
Flynn alihusishwa katika uchunguzi wa FBI uliofanyika 2016, lakini alianza kuchunguzwa na shirika hilo baada ya kukana hadharani alizungumzia vikwazo vya Marekani dhidi ya Urusi na balozi wa Urusi Sergey Kislyak baada ya uchaguzi wa Trump. FBI ilikuwa na ushahidi wa mawasiliano ya Flynn yaliorekodiwa.
Flynn alikuwa bado hajaajiriwa na utawala mpya wakati alipokuwa akizungumza kupunguza makali ya vikwazo hivyo.
Hatua ya kutaka kuondoa mashtaka hayo imezua okosoaji ikiwemo kutoka kwa wanachama wa Democrats katika bunge la Congress.
Uongozi wa idara hiyo uliopo umechukua hatua zisizo za kawaida kuwalinda wandani wa rais huyo na kuwaadhibu mahasimu wake, waliandika.
''Kwa maoni yetu , kesi kama hizo zinawakilisha mfumo wa haki uliozorota katika idara ya haki ikimaanisha kwamba kuna upendeleo wa kisiasa kama sio ufisadi wa moja kwa moja''.

Je shutumu za Trump kwa Obama zina umuhimu wowote?

Rais huyo kwa muda mrefu amechukulia uchunguzi wa Urusi kuingilia uchaguzi wa urais wa Marekani 2016 kama jaribio la kuhujumu uhalali wa urais wake.
Huku uchunguzi ukibaini kwamba baadhi ya maafisa wa FBI wanaochunguza Urusi , walishtumu na kukosoa kwa kibinafsi ugombea wa Trump, anahisi kuhalalishwa.
Maoni haya yameungwa mkono na Mkurugenzi wa zamani wa shirika la FBI James Woy, Mkurugenzi wa zamani wa Ushauri wa Kitaifa James Clapper na sasa Obama mwenyewe amemkosoa sana Trump, sera zake na urais wake.

Trump na Obama

Katika miezi ya mwisho ya 2016, serikali ya Marekani ilikuwa ikipokea maonyo kutoka kwa vitengo vyake vya ujasusi kuhusu juhudi za Urusi kuharibu uchaguzi mkuu wa 2016 - juhudi ambazo mtaalam maalum aliyekua akiongoza uchunguzi huo Robert Mueller alielezea zaidi.


ADVERTISEMENT


Pia alitoa ushahidi kuhusu mawasiliano kati ya wanachama wa timu ya kampeni ya Trump na raia wa Urusi. Uchunguzi huo ulianzishwa ili kuchunguza mawasiliano na vitendo vyao.
Maafisa waliokuwa katika utawala wa rais Obama , Shirikja la FBI na Ikulu ya Whitehouse imeendelea kutazama vitendo hivyo walivyochukua kutokana na ushahidi huo kama wa sawa.
Trump na wafuasi wake wanachukulia madai hayo kama ushahidi wa kufunika makosa.
Haitashangaza iwapo utaona mambo mengi yakifanyika katika wiki chache zijazo, zijazo, Trump alisema katika ofisi yake aiku ya Alhamisi baada ya kubaini kuhusu habari za Flynn.
Mgogoro kuhusu Flynn huenda ndio umeanza kualika maua.

Post a Comment

0 Comments