Bomu laua wanajeshi 7 wa Misri kaskazini mwa nchi hiyo

Wanajeshi saba wa Misri wameuawa baada ya bomu kuripuka wakati gari lao lilipokuwa linapita njiani katika eneo la Sinai la kaskazini mwa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Televisheni ya al Jazeera ya Qatar imetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, wanajeshi saba wa Misri wameuawa kwa bomu katika makao makuu ya eneo la Sinai la kaskazini mwa Misri katika shabulio la kulipiza kisasi lililofanywa na magenge ya kigaidi na ya ukufurishaji.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika kipindi cha wiki moja iliyopita, jeshi la Misri limefanya mashambulizi ya angani na ardhini dhidi ya maficho ya magenge ya kigaidi katika eneo la Sinai na kuua wamagaidi wasiopungua 19.


Katika operesheni hiyo, wanajeshi wa Misri wamekamata mikanda iliyoshehenezwa mabomu na silaha za kila namna katika maficho ya magaidi hao.

Kwa miaka kadhaa sasa jeshi la Misri linaendesha opereseheni za kupambana na magenge ya kigaidi na ya ukufurishaji hasa katika eneo la Sinai la kaskazini mwa nchi hiyo.

Magenge ya kigaidi yenye ngome zao katika jimbo la Sinai Kaskazini, huko kaskazini mwa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika ni hatari sana hasa genge linalojiita "Answar Bayt al Muqaddas" ambalo baada ya kutangaza utiifu wake kwa genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) limebadilisha jina na kujiita "Wilaya ya Sinai."

Soma Habari zote hapa->

Post a Comment

0 Comments