Burundi kutangaza matokeo ya awali ya uchaguzi leo



 Kulingana na mwaliko wa tume hiyo kwa vyombo vya habari, tangazo hilo la matokeo ya awali litatolewa saa nane mchana majira ya Burundi, na matokeo kamili yatatangazwa Juni 4.


 Matokeo ya muda yaliyochapishwa na shirika la habari la taifa yamemuonyesha Ndayishimiye akiongoza na asilimia 80 ya kura zilizopigwa.

Mpinzani wake mkuu, Agathon Rwasa ambaye mikutano yake ya kampeni ilihudhuriwa na umati mkubwa aliambulia asilimia takribani 20, huku wagombea wengine 5, kwa pamoja wakimudu asimilia moja. Msemaji wa Rwasa amesema kilichotokea ni mpango uliosukwa vyema na chama tawala wa kung'ang'ania madarakani.

Post a Comment

0 Comments