tangazo

Chama cha TLP chamuunga mkono Rais Magufuli kwenye uchaguzi ujao

Chama Cha Tanzania Labour Party-TLP kupitia Mkutano Mkuu wake Uliofanyika jijini Dsm leo Umekubaliana Kutosimamisha Mgombea Urais Kupitia Chama hicho na Kumuunga Mkono Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika Uchaguzi Mkuu Unaotarajiwa Kufanyika Oktoba Mwaka huu .

Akizungumza Wakati akitoa Maazimio yaliyofikiwa na Mkutano Mkuu wa TLP M/kiti wa Chama Cha TLP Bw. Agustine Lyatonga Mrema amesema Azimio la Kumuunga Mkono Dkt. Magufuli katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba Mwaka huu unatokana na Kazi Kubwa aliyoifanya katika Miaka 5 ya awali ya Kuwatumikia wananchi kwa Weledi,haki na wajibu na kuelezea kuwa Chama Hicho kitakuwa tayari Kusimama katika Majukwaa kuelezea kazi kubwa Iliyofanywa na Rais Magufuli.

Aidha Bw. Mrema amesema Chama chake hakitakuwa tayari kuwa sehemu ya Vyama vinavyotumika na Wasioitakia Mema nchi na kueleza wasiwasi wake katika Kuungana na vyama vingine kuelekea katika Uchaguzi Mkuu Ujao.

Katibu Mwenezi wa CCM Bw. Humphrey Polepole ambae alialikwa katika Mkutano huo Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM amekipongeza chama cha TLP kwa Uamuzi wake wa Kumuunga Mkono Dkt. Magufuli lakini pia Kwa Ukomavu katika Demokrasia.

Wakati huo huo Bw. Pole pole amewataka Watanzania kuendelea kufanya kazi na kuondoa hofu wakati wakiendelea kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona.

Post a Comment

0 Comments