Chama kikuu cha Wakulima wa Kahawa Kalagwe chapanga kukusanya tani 45,000, ya Kahawa

Chama kikuu Cha Ushirika kinachosimamia  wakulima wa Kahawa Wilaya ya Karagwe KDCU kimesema kwa msimu ujao wanatarajia kukusanya tani 45, 000 za Kahawa bora, kutoka maeneo mbali mbali hapa nchini, sambamba na kuwahakikishia wakulima bei bora ya mazao yao.

Sambamba na hilo chama hicho kimeipongeza Serikali kwa kuendelea kusimamia kuhakikisha wakulima wa kahawa wanapata stahiki zao, baada ya Naibu Waziri wa Kilimo Husein Bashe hapo jana kufanya kikao na wadau wote wa zao la kahawa ili kuhakikisha wakulima ananufaika na nguvu zao.

Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na  Meneja wa KDCU Oscar Dominic, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na zao hilo la biashara ambalo linalolimwa maeneo mbalimbali hapa nchini.

 Amesema Kahawa hiyo wanaamini itawanufaisha wakulima kutokana na bei ambazo wanaamini zitakwenda kuwanufaisha wakulima wa zao hilo kutokana na bei walizopanga kuwapatia.

"Tunatarajia kukusanya kiasi hicho cha kahawa ambacho mwaka huu tunaamini wakulima watafaidika na zao hilo, " amesema Dominic.

Kuhusu  bei ya Kahawa amesema msimu huu wanatarajia kuuza kahawa kwa sh 1300 mpaka 1400 ikiwa ni agizo kutoka serikali ya kutaka zao hilo liuzwe kwa bei nzuri ili wakulima waweze kunufaika.

Amewataka wakulima wawe na imani na chama hicho na  watarajie vitu vizuri kutoka chama hicho ambapo watapata bei nzuri ili wafaidike katika zao hilo  wakulima wapate faida na sihasara kama ilivyozoeleka.

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa KDCU Anselimu Kabatereine amesema mwaka Jana walitarajia kuvuna tani 35, 000  ambapo walifanikiwa kuvuna tani 30, 000 ambapo ni sawa na asilimia 88.

"Tumejipanga kukusanya tani 45, 000 ambazo tutakuwa tumefikia malengo tuliyojipangia, tofauti na mwaka jana tulikusanya tani 30, tofauti na malengo" amesema kibatereine.


Amesema maandalizi ya msimu ujao tayari umeanza, na maandalizi take yamekamilika, na Sasa wakala wa vipimo anapitia mizani yote ili wakulima wasipunjwe wakati wa kuuza mazao yao.

Amesema Kama chama  wamejipanga kuwasaidia wakulima kwa kutafuta mbegu bora ili wapate mazao mengi msimu wa kilimo ukifika.


ADVERTISEMENT

Post a Comment

0 Comments