tangazo

China yaitaka Marekani kuondoa vikwazo kampuni za teknolojia


China imeitaka Marekani kuondoa vikwazo dhidi ya mauzo ya nje ya kampuni za nchi hiyo katika duru ya hivi karibuni na mzozo unaozidi kutokota kuhusu teknolojia, usalama na haki za binadamu.

Wizara ya mambo ya nje ya China imeutuhumu utawala wa rais Donald Trump kwa kuingilia masuala ya ndani ya China kwa kuzijumlisha kwenye orodha mbaya, kampuni nane zinazotuhumiwa kushiriki katika ukandamizaji katika mkoa wa Xinjiang wenye Waislamu wengi.

Washington pia imeweka udhibiti katika upatikanaji wa teknolojia ya Marekani kwa kampuni 24 na taasisi zenye mafungamano na serikali, ambazo imesema huenda zinashiriki katika ununuzi wa bidhaa zinazoweza kuwa na matumizi ya kijeshi.

Msemaji wa jeshi la China Zhao Lijian amesema uamuzi huo wa Marekani unakiuka utaratibu wa msingi wa mahusiano ya kimataifa na kudhuru maslahi ya China.

Post a Comment

0 Comments