China yatoa orodha ya bidhaa za Marekani zitakazosamehewa ushuru

China leo imetoa orodha ya bidhaa 79 kutoka Marekani ambazo zitasamehewa ushuru katika vita vya kibiashara, siku moja baada ya Marekani kuondoa uwezekano wa kujadili tena mkataba wao wa awali wa biashara.

Orodha hiyo ya bidhaa ambayo imewekwa mtandaoni na tume ya ushuru wa forodha, inajumuisha madawa ya kuua vijidudu, maw ya nadra yenye madini ya chuma na vifaa vinavyotumika katika sekta ya umeme.

Bidhaa hizo zitasamehewa kutozwa ushuru wa kulipizana kisasi kwa kipindi cha mwaka kuanzia Mei 19. Awali China ilitangaza mwaka mmoja wa msamaha wa kodi kuanzia Februari 28, ukihusisha bidhaa 65 kutoka Marekani, ikiwemo vifaa vya ndege na matibabu.

Utawala wa Trump ulikubali kuahirisha kuongezeka kwa ushuru wowote wakati China ikiahidi ongezeko la dola bilioni 200 katika ununuzi wa bidhaa za Marekani kwa miaka miwili.


ADVERTISEMENT

Post a Comment

0 Comments