tangazo

China yawaonya waandamanaji wa HongKong

China imewaonya waandamanaji wa Hong Kong kwamba haitowaruhusu kuanzisha tena vurugu na maandamano katika jimbo hilo lenye mamlaka yake ya ndani ambalo lilikumbwa na maandamano makubwa kwa kipindi cha miezi kadhaa mwaka jana.

Hatua za kukamatwa kwa waandamanaji wengi na kupigwa marufuku kwa mikusanyiko katika kipindi cha janga na virusi vya Corona, zimelivunja vuguguvu la maandamano lakini maandamano ya makundi madogo madogo yamekuwa yakifanyika katika wiki za karibuni wakati hofu ya janga la Corona ikianza kuondoka.

Baraza la serikali ya Hong Kong limetowa taarifa yake likisema serikali kuu mjini Beijing haiwezi kukaa na kuangalia vurugu za makundi hayo ya waandamanaji.

Taarifa hiyo imekuja baada ya uchumi wa Hong Kong kuonesha umeathirika vibaya.

Post a Comment

0 Comments