Daktari wa Uturuki afariki kwa Covid-19 nchini Marekani

Daktari  mmoja kutoka Uturuki amefariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona nchini Marekani.

Halil Sina Zaim, daktari kutola nchini Uturuki ameripotiwa kufariki kutokana na mamabukizi ya virusi vya corona katika jimbo la New Jersey nchini Marekani.

Daktari Halil Sina Zaim aliambukiwa  virusi hivyo akiwa  katika kutekeleza wajibu wale mjini New Jersey nchini Marekani.

Daktari  mtaalamu  wa moyo aliekuwa akiishi katika mji wa Mountain Lakes  alikuwa akipatiwa matibabu ya covid-19  kwa muda wa siku kadhaa  zilizopita.

Zaim  amezikwa mjini New York.

Miti itapandwa na shirika la wauguzi wa Uturuki na Marekani kwa ajili ya kumuenzi Daktari Zaim ambae amezaliwa mjini Ankara mwaka  1951.

Daktari  huyo alikuwa akiendelea na masomo na utafiti nchini Canada, Uswisi,  Uturuki na Marekani.

Nchini Marekani , waturuki 23  wamefariki kutokana na virusi vya corona, 19 New York, watatu katika jimbo la Chicago na mmoja Florida .


ADVERTISEMENT

Post a Comment

0 Comments