tangazo

Diaimond aanza kulipa kodi ya miezi mitatu kwa kaya 57

Mkurugenzi wa kampuni ya Wasafi, msanii Diamond Platnumz ametoa msaada wa kodi ya pango kwa watu 57 ambao ni wajane, walemavu pamoja na wasiojiweza.

Msaada huo ni awamu ya kwanza katika ile dhamira yake ya kusaidia kodi ya pango kwa kaya 500 nchini zilizoathirika kiuchumi na janga la mlipuko wa virusi vya Corona.
Diamond Platnumz ametoa msaada huo leo katika makao makuu ya ofisi za kampuni ya WasafiMedia baada ya watu zaidi ya 100 kujitokeza ofisini hapo ambapo familia 57 zimeweza kupata msaada huo.

Kufuatia jambo hilo, familia zilizobakia kwenye orodha ya kaya 500 ni 443 ambapo mchakato unaendelea kwa ajili ya kuzipata kaya za wajane, walemavu na wasiojeweza.

Post a Comment

0 Comments