Dunia yaadhimisha miaka 75 ya kumalizika kwa Vita vya Pili

Mkutano wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu maadhimisho ya miaka 75 ya kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia barani Ulaya ulishuhudia makabiliano kati ya Urusi na baadhi ya mataifa ya Ulaya, miito ya umoja kukabiliana na virusi vya corona na onyo la kuzuia kuenea kwa mzozo mpya wa kimataifa.

Takriban washirika 70, ikiwa ni pamoja na mawaziri 45 wa kigeni na wajumbe wakuu wa Umoja wa Ulaya, walihudhuria mkutano huo kuhusu mafunzo yaliopatikana kutoka kwa vita hivyo na njia za kuzuia maasi ya siku za baadaye na pia jukumu la Baraza hilo la Usalama, ulioandaliwa kwa njia ya video na Estonia inayoshikilia urais wa Baraza hilo mwezi huu.

Mkuu wa Sera za Nje za Umoja wa Ulaya, Josep Borell, amesema kuwa dunia inakabiliwa na mzozo mkubwa zaidi tangu kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia kutokana na virusi vya corona vinavyotingisha misingi ya kijamii.

Post a Comment

0 Comments