tangazo

Hakuna corona Korea Kaskazini

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameonekana mara chache hadharani ndani ya miezi miwili iliyopita na sasa inakaribia wiki ya 3 bila vyombo vya habari kuripoti tukio lolote akiwa hadharani, mwaka jana miezi kama hii (mitatu) alionekana hadharani mara 27.

Kuonekana hadharani mara chache kwa Kim Jong Un kipindi hiki kumeendelea kuibua maswali lakini majirani zake Korea Kusini wanasema huenda Kim anachukua tahadhari dhidi ya corona kwa kukwepa mikusanyiko, ingawa bado Nchi yake haijaripoti maambukizi ya corona hadi sasa.

Korea Kaskazini ni miongoni mwa Nchi ambazo taarifa zake huwa hazitoki kwa urahisi hadi pale wanapoamua kuzitoa wenyewe na hii inafanya kuwe na ugumu kwa Dunia kujua kinachoendelea kumuhusu Kim na hivyo kubaki na hisia zisizo na uthibitisho kuhusu sababu ya ukimya wake.

Post a Comment

0 Comments