tangazo

Harmonize azua msala Live mbele ya mkewe na Nicole

Kama ulifuatilia Instagram ya msanii Harmonize usiku wa jana Mei 6,2020, utakuwa uliona alivyokuwa Live kupitia "Insta Live" ambapo alimpigia simu video vixen ambaye ameshoot naye video ya bedroom Nicole Joy Berry na msanii wa filamu Jacqueline Wolper.

Wakati Harmonize yupo Live na Jacqueline Wolper, kulikuwa na mashabiki 5387 ambao walikuwa wanatazama, wengine wakicomment kutaka warudiane pia wengine walishangwazwa na tukio hilo la Harmonize kuwasiliana na EX wake hadharani.

Video ya pili kwenye "insta live" Harmonize alizungumza na mrembo Nicole Joy Berry, sasa katikati ya mazungumzo yao mke wa Harmonize Sarah aka-comment kwa kuandika "Baby nenda salimia Nicole nyumbani".

Baada ya comment hiyo Nicole Joy Berry akamjibu kwa kusema  "Sasa Sarah anaanza kuongea maneno mabaya unaona comment yake eti nenda salimia Nicole nyumbani, simuhitaji Harmonize nyumbani kwangu na sijampigia mwanaume wako yeye ndiyo amenipigia, mimi sipendi haya mambo anaanza kuleta habari gani, kwaheri nikibaki hapa mambo yatakuwa mengi".

Post a Comment

0 Comments