Hofu yatanda Asia wimbi la pili la maambukizi

Visa vipya vya maambukizi ya virusi vya corona vimejitokeza nchini China, Korea Kusini na Iran, hali inayotishia mafanikio yaliyopatikana dhidi ya virusi hivyo. Ujerumani nako kasi ya maambukizi imepanda tena.

Wakati idadi jumla ya watu walioambukizwa virusi vya Corona duniani kote ikipindukia milioni nne (4,000,000) mji wa Wuhan nchini China ulikoanzia mripuko huo kumeripotiwa kisa kipya kwa mara ya kwanza katika muda wa zaidi ya mwezi mzima. Wimbi jipya linaloonekana katika nchi za Asia linaaminika kuwa na chimbuko katika vilabu vya usiku vya nchini Korea Kusini.

Leo Jumapili, Korea Kusini imethibitisha visa vipya 34, idadi hiyo ikiwa kubwa zaidi kusajiliwa kwa siku moja kwa zaidi ya mwezi mzima.

Ijumaa iliyopita wahudumu wa afya walifanya juu chini kutafuta watu waliowasiliana na kijana wa miaka 29 aliyethibitika kuwa na virusi vya corona, ambaye anaripotiwa kuvitembelea vilabu vitatu vya usiku katika kitongoji cha Itaewon chenye shughuli nyingi za burudani katika mji mkuu, Seoul.

ADVERTISEMENT

Post a Comment

0 Comments