tangazo

Iran yasema itaendeleza shughuli zake za nyuklia


Iran imesema hii leo kwamba wataalamu wake wataendelea na shughuli za uendelezaji wa nishati ya nyuklia, licha ya vikwazo vya Marekani ilivyowawekea wanasayansi wake mapema wiki hii.

Kituo cha televisheni cha taifa kilinukuu taarifa ya idara ya nyuklia ya nchini humo, iliyosema maamuzi ya Marekani ya kuwawekea vikwazo wanasayansi wake wawili inaashiria mwendelezo wa tabia ya kichokozi.

Imesema vikwazo hivyo vitawafanya kuamua kuendelea na juhudi zao zaidi ya ilivyokuwa awali. Taarifa hiyo imesema vikwazo hivyo vinakiuka sheria ya kimataifa.

Siku ya Jumatano waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo aliwawekea vikwazo maafisa hao wawili wa shirika la atomiki la Iran Majid Agha'i na Amjad Sazgar wanaojihusisha na utengenezaji wa uzalishaji wa vyombo vinavyorutubisha madini ya urani.

Post a Comment

0 Comments