tangazo

IS yamshambulia waziri mkuu wa Iraq

Kundi la wanamgambo linalojiita Dola la Kiislamu, IS limeshambulia waziri mkuu mpya wa Iraq kwa kumuita "kibaraka wa Marekani".

Aidha IS limekosoa hatua ya kufungwa kwa eneo takatifu zaidi la ibada la Kiislamu katika mji mtakatifu wa Mecca, nchini Saudi Arabia, katika hatua za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.

Kwenye ujumbe wa sauti uliotolewa na kundi hilo na kusomwa na msemaji wake mkuu Abu Hamza al-Qurayshi jana usiku, alihoji kwa nini misikiti inafungwa na watu wanazuiwa kuswali kwenye msikiti mkuu wa Mecca, akigusia kuwa Waislamu wana kinga na virusi vya corona, na kutoa mwito kwa wanamgambo hao kuanzisha mashambulizi ya kila siku nchini Syria, Iraq na mataifa mengine.

Ujumbe huu wa tatu kutolewa na kundi hilo tangu al-Qurayshi aliposhika madaraka hayo.

Waziri mkuu wa Iraq Mustafa al-Khadhimi, mkuu wa zamani wa idara ya kijasusi aliyeungwa mkono na Marekani aliingia mamlakani mapema mwezi huu.

Post a Comment

0 Comments