tangazo

Ivory Coast yajiondoa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu

Ivory Coast imetangaza kujiondoa kwake katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu.

Nchi hiyo imejiondoa ikidaikwamba Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu imedhoofisha uhuru wake.

Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ni mahakama ya kimataifa iliyoanzishwa na nchi za Afrika ili kuhakikisha ulinzi wa haki za binadamu na watu barani Afrika.

Wiki iliyopita, mahakama hiyo iliiamuru Ivory Coast isimamishe hati yake ya kukamatwa kwa Guillaume Soro na kuwaachilia ndugu zake 19 ambao walikuwa wamefungwa kwa miezi kadhaa.

Sidi Tiemoko Toure, msemaji wa serikali na waziri wa mawasiliano wa Ivory Coast amesema kuwa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu imedhoofisha mamlaka, uhuru na mfumo wa haki wa Ivory Coast.

Kibali cha kukamatwa kilitolewa kwa Soro - spika wa zamani wa bunge - baada ya kutangaza kuwania katika uchaguzi wa rais wa Oct. 31.

Siku ya Jumanne, Soro alihukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani.

Soro, 47, ambaye pia ni waziri mkuu wa zamani, alipatikana na hatia ya kuficha na kutapeli wa fedha za umma.

Kesi yake ilisikilizwa mjini Abidjan bika kuwepo mawakili wake.

Wiki iliyopita, Benin, nchi nyingine ya Afrika Magharibi pia ilitangaza kwamba inajiondoa kutoka kwenye itifaki ambayo inaruhusu raia wa nchi kukata rufaa moja kwa moja katika Mahakama ya Afrika.

Mahakama hiyo iliitaka Benin isimamishe uchaguzi wa manispaa wa Mei17, 2020 baada ya kiongozi wa upinzani kukata rufaa.

Itifaki ya Uanzishwaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ilipitishwa Ouagadougou, Burkina Faso, mnamo Juni 9, 1998 na ilianza kutumika mnamo Januari 25, 2004.

Post a Comment

0 Comments