tangazo

Jakaya Kikwete amzungumzia Marehemu Augustine Philip Mahiga aliyefariki jana

Makamu wa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo Jumamosi ataongoza mazishi ya aliyekuwa waziri wa Sheria na Katiba Dr. Agustine Mahiga ambae alifariki jana Ijumaa jijini Dodoma, baada ya kuukua kwa muda mfupi.
Dr. Mahiga atazikwa kwao huko Mkoani Iringa.
Augustine Philip Mahiga, ni moja ya wanadiplomasia mahiri kuwahi kutokea nchini Tanzania...Balozi Mahiga, mwanadiplomasia nguli aliyehudumu kwa miongo mitano
Pia ni moja kati ya watu wachache amabao wamefanya kazi katika ngazi za juu na awamu zote tano za serikali ya Tanzania kutoka kwa rais wa kwanza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mpaka awamu hii ya rais John Pombe Magufuli. Rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alimfahamu na kufanya kazi na Dkt. Mahiga anamzungumzia...

Post a Comment

0 Comments