tangazo

Je masharti mapya ya mechi yako vipi uwanjani ?

Borussia Dortmund iliwafunga wapinzani wao Schalke 4-0 huku wachezaji wakisherehekea magoli hayo kwa kugongana visukusuku
Ligi ya kandanda nchini Ujerumani iliendelea siku ya Jumamaosi na kutoa ishara za jinsi ligi ya Premia na ligi nyengine kuu zitakavyochezwa wakati zitakaporejea.
Ligi ya taifa la Korea Kusini ilianza wikendi iliopita , huku ligi ndogo ndogo kama ile ya Belarus na Nicaragua zikiendelea bila wasiwasi.
Je mechi zilichezwaje mwezi Mei 2020- zilichezwa bila mashabiki mbali na masharti ya kutokaribiana- je ilikuwaje?

Vipimo vya kuchunguza joto, huku mabasi kadhaa na mipira ikinyunyiziwa dawa za kuuwa virusi.

ishara ya picha ya kuosha mikono katika uwanja wa klabu ya RB leipzig UjerumaniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionVideo hii katika klabu ya RB Leipzig iliwataka watu kuosha mikono
Timu ziliwasili katika mabasi kadhaa ili wachezaji wasikaribiane wakati wa safari ya kuelekea uwanjani .
Wachezaji na wafanyikazi walikuwa wamewekwa katika karantini katika hoteli za timu hizo wiki yote na mara kwa mara walifanyiwa vipimo vya virusi vya corona.
Wakati walipokuwa wakiondoka katika basi walivalia barakoa wakielekea uwanjani.
Watu wengine waliokuwa wakihudhuria mechi hiyo , ikiwemo vyombo vya habari , walichunguzwa kwa vipimo vya joto kabla ya kuruhusiwa kuingia.
Mashabiki hawakuruhusiwa kuingia kutazama mechi viwanjani hivyobasi hakuna mashabiki waliowasili katika uwanja.
Ni watu 213 pekee walioruhusiwa uwanjani - 98 kandokando ya uwanja , - kama vile wachezaji , makocha na wavulana wanaorudisha mpira uwanjani na watu 115 katika maeneo ya mashabiki kama vile maafisa wa usalama , maafisa wa afya na wanahabari.
Watu wengine 109 wakiwemo walinda amani na wasimamizi wa Video zinazomsaidia refa VAR waliruhusiwa kandokando ya uwanja.
Mipira ilinyunyiziwa dawa ya kuuwa virusi na vijana wanaotumika kuingiza mipira uwanjani kabla na wakati wa kipindi cha mapumziko.
Vijana wa kuingiza mipra uwanjani wakinyunyizia mipira dawa ya kuuwa virusi.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKulikuwa na mipira 30 ilioandaliwa kwa mechi , kila mmoja ukiwa umenyunyiziwa dawa na vijana wakurudisha mipira uwanjani na kuwekwa katika eneo moja badala ya kuwapatia wahezaji.

Wachezaji wa ziada kutokaribiana walikokaa

Wachezaji wote wa ziada walikaa katika viti huku kukiwa na umbali wa mita moja na nusu katika yaoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWachezaji wote wa ziada walikaa katika viti huku kukiwa na umbali wa mita moja na nusu katika yao
Wachezaji wa ziada na makocha walivalia barakoa na kukaa mbalimbali katika viti vyao.
RB Leipzig ambayo ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya klabu ya Freiburg iliwawekea ngazi wachezaji waende katika viti vyao katika standi zao.
Makocha waliruhusiwa kuingia bila barakoa ili kuweza kutoa maelezo kwa wachezaji wao.
Wachezaji wa ziada walitoa barakoa zao ili kupasha misuli na wakati wa mabadiliko wachezaji waliokuwa wakitoka walipatiwa barakoa kabla ya kukaa katika viti vyao.

Walisalimiana kwa kutumia visukusuku vya mikono badala ya kukumbatiana

Baadhi ya magoli ylisherehekewa bila wachezaji kukaribianaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBaadhi ya magoli ylisherehekewa bila wachezaji kukaribiana
Wachezaji wa klabu ya Hertha Berlin wakisherhekeaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption... lakini wengine walishindwa kufuata masharti ya kutokaribiana mna waliweza kusherehekea kwa pamoja
Mchezo wenyewe haukuwa tofauti na ule wa kawaida huku wachezaji wakikabiliana na kukabana mbali na ufungaji wa magoli 16 katika mechi zote sita zilizochezwa siku ya Jumamosi.
Lakini wachezaji hawakukaribiana wakati wa kusherehekea magoli yaliofungwa kama ilivyo kawaida - ambapo wachezaji hukumbatiana .
Walisalimiana kwa kutumia viwiko vya mikono yao badala ya kukumbatiana.
Hatahivyo baadhi ya magooli hususan yale yaliofungwa na wachezaji wa Hertha Berlin katika ushindi wao wa 3-0 dhidi ya Hoffenheim yalisherehekewa kama kawaida.
Hertha Berlin haitaadhibiwa kwa kuwa ligi hiyo ya Ujerumani ilitoa agizo hilo kama muongozo na sio sheria.
Huku ikiwa ni watu wachache pekee wanaopiga kelele katika viti, watazamaji wa runinga waliweza kuwasikia wachezaji na wakufunzi wao wakizungumza pamoja na sauti ya mpira ukipigwa na kupiga wavu.
Timu ziliruhusiwa kutumia wachezaji watano wa ziada katika mechi moja - kitu ambacho ligi nyengine zitalazimika kufaya zitakaporudi .
Hivyobasi klabu ya Schalke , katika mechi yao dhidi ya Borrusia Dortmund walioshindwa 4-0 , waliweza kufanya mabadiliko mawili wakati wa mapumziko na wengine watatu baada ya mapumziko hayo.

Wachezaji baadaye walipongeza standi tupu bila mashabiki

Wachezaji wa Borussia Dortmund walikwenda hadi katika standi ya mashabiki wao na kusherehekea ushindi waoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWachezaji wa Borussia Dortmund walikwenda hadi katika standi ya mashabiki wao na kusherehekea ushindi wao
Baada ya kipenga cha mwisho wachezaji wa Borussia Dortmund walienda katika standi ya mashabiki wao kusherehekea mbele ya standi zisizo na mashabiki hao inayojulikana kama ukuta wa manjano inayobeba mashabiki 25,000.
Wachezaji wa Wolfsburg walisalimiana na marefa wa mechi hiyo kwa kugongana miguu baada ya mechiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWachezaji wa Wolfsburg walisalimiana na marefa wa mechi hiyo kwa kugongana miguu baada ya mechi
Wachezaji wa Wolfsburg waligongana viatu na marefa na manaibu wao , badala ya maamkuzi ya kawaida kufuatia ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Augsburg.
Wachezaji na maneja walihojiwa na maripota wa runinga wakiwa mbali huku mahojiano baada ya mechi yakifanywa kupitia mikutano ya video .
Mshambuliaji wa RB Leipzig Yussuf Poulsen alihojiwa akiwa mbaliHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji wa RB Leipzig Yussuf Poulsen alihojiwa akiwa mbali
Je mashabiki walisusia mechi?
Police made sure fans could not congregate outsideHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPolice made sure fans could not congregate outside
Sababu mojawapo ya mechi za ligi ya premia kuchezeshwa katika viwanja visivyopendelea upande wowote ni kujaribu kuzuia mikutano ya mashabiki nje ya viwanja vyao wakati wa mechi.
Lakini hilo halikuonekana kuwa suala nyeti nchii Ujerumani siku ya Jumamosi.

Iwapo huwezi kusherehekea kila kitu hakifurahishi.

Baada ya sare ya bila magoli na Paderborn , mkufunzi wa klabu ya Fortuna Dusseldorf Uwe Rosler alisema: Siku haikuwa ya kawaida.
''Mimi ni mtu wa hisia , napenda kumkumbatia mchezaji mikononi mwangu kitu ambacho nilishindwa kufanya hii leo''.
Mkufunzi wa Dortmund Luvcien favre alisema: hakuna kelele. Unashambulia goli, unapiga pasi nzuri, unafunga na hakuna kinachotokea. Ni kitu cha kushangaza kwa kweli.

Post a Comment

0 Comments