tangazo

Kauli ya JPM kurejesha ligi kuu yamkosha Haji Manara

Hapo jana Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alisema anafikiria siku zijazo huenda akaruhusu kurejea kwa Ligi Kuu soka Tanzania Bara na michezo mingine kwa kile alichokisema ili kuwapa nafasi wananchi kutazama michezo hiyo, kwenye TV.

Rais Magufuli alizungumza hayo jana Aprili 22, 2020 mara baada ya kumuapisha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mbunge wa Iramba Magharibi) kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, hafla iliyofanyika Wilayani Chato Mkoani Geita.

Sasa Msemaji wa Simba SC, Haji Manara ameeleza kufurahishwa na kauli hiyo ya Rais Magufuli kwa kueleza wapenda michezo wengi nchini walikuwa wakiiongojea.

“Leo (jana) umeusuuza moyo wangu, hakuna kitu watu wa mpira tulikuwa tunakingoja kama kauli yako ya leo. Wabongo ndio muelewe Power of Football nchini, Thanks My President.” ameandka Haji Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Ikumbukwe toka Machi 17 mwaka huu Serikali ya Tanzania kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ilitangaza kusimamisha Ligi Kuu Tanzania Bara kwa muda kutokana na kujilinda na maambukizi ya virusi vya Corona.

Post a Comment

0 Comments