tangazo

Kauli ya Rais Magufuli baada ya kumuapisha Mwigulu Nchemba

''Waziri Mwigulu Nchemba nimekuapisha hapa uende mkacheki vizuri maabara inayohusika na upimaji ncorona kuna vitu vingi haviko sawa ,kulikuwa na kila sikuni positive ,namshukuru sana katibu mkuu

Tulifanya mambo kadhaa ili kujua ubora wa maabara tukapeleka sampuli za wanyama,ndege na vitu vingine bila wao kujua ,tukazipa majina ya watu, tukapeleka sampuli ya mbuzi akawa positive, mapapai nayo positive, maana yake mbuzi ,mapapai yote yana corona

Ugonjwa mpya unapoingia watu huwa na uoga,UKIMWI ulipoingia kupitia Kagera ilikuwa ukikutana na mtu mwenye UKIMWI unamkwepa, kulikuwa na surua wakati ninaingia ukiwa na surua hakuna anaekutazama , kwa hio niwahakikishie watanzania  ,ugonjwa huu utapita,tupunguze hofu''.

Post a Comment

0 Comments