Kenya: Idadi ya wagonjwa wa corona yaongezeka hadi kufikia 700

Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona nchini Kenya imeongezeka hadi 700 baada ya wagonjwa wapya 28 kuthibitishwa katika kipindi cha saa 24.

Katibu mtendaji katika wizara ya Afya Rashid Aman amesema kwamba kati ya wagonjwa hao wapya 10 wanatoka Momabasa , 9 kutoka kajiado na 7 kutoka Nairobi huku 2 wakitoka Wajir.

Wagonjwa wote tisa kutoka Kajiado ni madereva wa malori ya masafa marefu ambao walikuwa wanarudi kutoka Tanzania katika mpaka wa Namanga.

Jumla ya sampuli 841 zilifanyiwa vipimo katika kipindi cha saa 24 zilizopita

Afisa huyo wa afya alitangaza wagonjwa wengine 12 waliopona na hivyobasi kufanya idadi ya wale waliopona kufikia 251.

Amesema kwamba wagonjwa wengi ambao wamefariki na ugonjwa huo katika kaunti ya Mombasa ni watu wenye umri mkubwa.

Hatahivyo Aman alitangaza kifo kimoja zaidi mjini Nairobi na hivyobasi kuongeza idadi ya waliofariki kutokana na ugonjwa huo kufikia watu 23.

Aman ameongezea kwamba idadi ya kaunti zilizoathiriwa na ugonjwa huo zimeongezeka.

''Ni wazi kwamba ugonjwa huu utasambaa katika taifa zima . huku tukiingia katika mwezi wa tatu ni lazima tulindane'', alisema.

Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari siku ya Jumatatu , afisa huyo alisema kwamba lengo la serikali ni kupunguza usambazaji katika jamii.

Aman amewataka Wakenya kuripoti katika hospitali zilizo karibu nao kuhakikisha kwamba wanasaidika kabla ya dalili hizo kuwa mbaya.

ADVERTISEMENT

Post a Comment

0 Comments