Kenya na Uganda zakabiliwa na tatizo la kitaifa la kusambaza umeme

Mataifa ya Afrika Mashariki ya Kenya na Uganda yanakabiliwa na tatizo la kitaifa la kukatika kwa umeme.

Kupitia mtandao wa Twitter, Shirika la Umeme la Kenya, Power and Lighting, limesema kuwa limepoteza uwezo wa kusambaza umeme kwenye gridi ya taifa kutokana na matatizo katika mfumo wake

.Katika taifa jirani la Uganda, shirika la kusambaza umeme, UETCL, pia lilitangaza tatizo la kitaifa la kusambazwa kwa nguvu za umeme hii leo asubuhi.Katika taarifa, kampuni ya Umeme Limited inayopata umeme wake kutoka kwa shirika la UETCL, imesema kuwa maafisa wa shirika hilo wanashughulikia tatizo hilo kuhakikisha limerekebishwa mara moja.

Bado haijabainika iwapo matatizo hayo katika mataifa hayo mawili yanaingiliana.

Post a Comment

0 Comments