tangazo

Kenya yatangaza idadi kubwa zaidi ya wagonjwa wa corona kwa siku


Waziri wa Afya nchini Kenya Mutahi Kagwe leo Jumatano Mei 27 ametangaza watu 123 zaidi kuambukizwa virusi vya corona.

Hiyo ndiyo idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya corona kuwahi kutangazwa kwa siku moja nchini humo tangu ugonjwa huo uingie Kenya mwezi Machi.

Mpaka kufikia sasa Kenya imethibitisha watu 1,471 kuambukizwa virusi hivyo.

Wagonjwa hao wapya wanatokana na sampuli 3,077 ambazo zimepimwa hivi karibuni.

Waziri Kagwe pia ametangaza watu watatu zaidi wamefariki kutokana na corona katika saa 24 zilizopita na kufanya watu waliopoteza Maisha kutokana na virusi hivyo nchini Kenya kufikia 55.

Kati ya wagonjwa hao wapya 123, jiji la Nairobi linaongoza kwa kuwa na wagonjwa 85 ikifuatiwa na 23 wa Mombasa.

Waziri Kagwe ameeleza kuwa ongezeko hilo la wagonjwa linatokana na matumizi ya usafiri wa umma ambao ndio kimbilio la wengi nchini humo.

Post a Comment

0 Comments