tangazo

Kipa wa Yanga akwama nchini Kenya

FAROUK Shikalo, kipa namba moja wa Yanga amekwama nchini Kenya ambako alikwenda kwa ajili ya mapumziko yaliyotolewa na Serikali kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wachezaji wote wa kigeni kwa sasa wapo Bongo isipokuwa Shikalo ambaye yupo Kenya.

"Wachezaji wote wakigeni wapo hapa Bongo kwa sasa isipokuwa Shikalo ambaye yupo Kenya alikokwenda kwa ajili ya mapumziko ila kwa sasa mipaka imefungwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona," .

Ligi Kuu Tanzania Bara ilisimamishwa Machi 17 kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vimekuwa ni janga la dunia kwa sasa.

Post a Comment

0 Comments