tangazo

KKKT wazindua mpango wa kuingia vijijini kuelimisha jamii kupambana na Corona

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kusini Kati wilayani Makete mkoani Njombe,kwa kushirikiana na Madhehebu mengine wilayani humo,wamezindua mpango Maalum wa kudhibiti na kupambana na virusi vya Corona (COVID-19) na kufika kila kijiji ndani ya wilaya ili kutoa elimu ya kupambana na kirusi Corona.

Askofu wa Dayosisi ya Kusini kati Wilson Sanga amesema tangu tatizo hilo lilipoingia nchini,Kanisa limeungana na serikali kuunga mkono juhudi za Serikali katika vita dhidi ya Corona.

“Tangu tatizo hili lilipoingia kanisa la Kilutheri pamoja na vyama vya wamisioni Ulaya na Amerika,Jumuiya ya Kikristo Tanzania vyote vimeungana na serikali kuunga mkono katika vita dhidi ya Corona,hii ikiwa ni pamoja na baadhi ya vyama kutoa fedha au kuruhusu fedha ambayo Dayosisi ilipanga kutumia kwa miradi maalum kwamba sasa fedha hiyo inaweza ikatumika katika mpango wa kupambana na virusi vya Corona.Hivyo Dayosisi imeamua kunzisha mpango huu ambao katika hatua za awali unakadiliwa kutumia kiasi cha Milioni 15”alisema Askofu Wilson Sanga

Akizungumza kwa niaba ya mganga mkuu wa wilaya ya Makete,Bonifas Sanga ambaye ni afisa afya wa wilaya,amesema awali kabla ya kuruhusu kanisa kuanza mpango huo,serikali kupitia idara ya afya imefanikiwa kudhibitisha ubora zikiwemo Barakoa na vifaa vingine vitakavyotumika wakati wa uelimishaji vijijini pamoja na kugawa kwa makundi maalum.

“Nipende kupongeza kwenye maeneo ambayo mnaanza kuhudumia hapa Makete wakiwemo Walemavu na wazee,na nitamke hapa kwamba vifaa vya barakoa vilivyoandaliwa na kundi hili vina ubora na vinaruhusiwa kutumika”alisema Bonifasi Sanga

Ronester Mgaya na Hekima Mgenzi ni baadhi ya walemavu wanaofanya shughuli za ushonaji wa Barakoa zilizokidhi vigezo katika kituo cha Udiakonia Tandala na kukubaliwa na wataalamu wa Afya Makete.Wameishukuru Dayosisi pamoja na serikali kuona umuhimu wa kuinusuru jamii ya Makete dhidi ya Corona.

Akizundua mpango huo Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Makete Francis Namaumbo kwa niaba ya mkuu wa wilaya.Amesema serikali serikali ya wilaya imeunda timu zinazotembea na kufuatilia kuhakikisha wananchi wananchi wanaendelea kufuata maelekezo huku akipongeza mpango huo wa kanisa.

“Kwa hiyo nanyi tuendelee kutoa maelekezo dhidi ya corona katika nyumba zetu na familia zetu na kila familia ikichukua tahadhari kwa asilimia mia tutakuwa salama”alisema Namaumbo

Aidha amewaasa wana Makete kufanya ajenda ya kupambana na virusi vya Corona kuwa ya Kudumu ili virusi visweze kuenea wilayani humo

Post a Comment

0 Comments