tangazo

Klabu za ligi ya Uingereza kujadiliana kuhusu uwezekano wa kurejea viwanjani

Klabu katika ligi kuu ya Uingereza zinatarajiwa kufanya mazungumzo leo kuhusu namna ya kumaliza msimu. Haya yanajiri huku mshambulizi wa Manchester City, Sergio Aguero, akikiri kuwa wachezaji wana wasiwasi kwamba wanaweza kuharakishwa kurudi viwanjani.

 Ligi hiyo ya Uingereza inakabiliwa na kitisho cha kupata hasara ya euro bilioni moja ikiwa mechi hazitachezwa tena kwa sababu ya janga la corona.

Suluhisho la hasara hiyo ni kuzicheza jumla ya mechi 92 ambazo zimesalia hata bila ya kuwepo mashabiki uwanjani.

 Lakini ligi hiyo inakumbwa na changamoto nyingi za kimkakati katika majaribio yake kutaka kurejea viwanjani mnamo wakati Uingereza ikiwa kati ya mataifa yaliyoathiriwa mno na janga la COVID-19.

Post a Comment

0 Comments