tangazo

Lema amjibu ndugai "Wabunge wa CHADEMA hawapelekeshwi"

Mbunge wa Arusha Mjini, kupitia CHADEMA, Godbless Lema, amesema kuwa kauli aliyoitoa Spika wa Bunge Job Ndugai, kwamba wabunge wa CHADEMA wanapelekeshwa, si ya kweli na aliitoa kwa dharula kwa kuwa chama chake kinaongozwa na watu wanaojielewa na hivyo hakuna mtu wa kumpelekesha mwenzake.

Mbunge Lema ameyabainisha hayo  kauli ya Rais Magufuli ya kuzuia Wabunge wote ambao wamegoma kuhudhuria Bunge kutolipwa posho, ambapo Lema amesema uhai ni kila kitu na Corona imeua mwanafamilia wake hivyo hawezi kuleta mzaha.

"Kwanza siyo kweli, Wabunge wa CHADEMA hawapelekeshwi na mtu yeyote na ukitaka kujua sisi tuna Wabunge ndani ya chama wawili wametangaza kuhamia NCCR na hujasikia chama kimekaa, lakini maelekezo yalitolewa siku ambayo Waziri Mahiga alikuwa amefariki hivyo ilikuwa ni kauli ya dharula, na ndiyo maana Mwenyekiti amesema tunaendelea kuitafakari" amesema Mbunge Lema.

Aidha Lema ameongeza kuwa kulingana na hali ya maambukizi ilivyo kwa sasa, imefikia hatua hata yeye hachangamani na familia yake kwa kuwa amejitenga kwenye chumba chake pekee lengo likiwa ni kuiweka salama familia yake.

"Mimi hapa ninapoongea kwenye familia yetu tayari kuna mtu amekufa na ugonjwa huu, mimi hatari nimeiona kwa kina sana, mimi nimekuja nyumbani nimejitenga chumba na watoto wangu na siumwi na nina mtazama mke wangu kama Dada yangu".

Post a Comment

0 Comments