tangazo

Ligi ya Bundesliga kurejelewa Mei 16, 2020

Mabingwa wa ligi hiyo Bayern Munich watacheza siku ya Jumapili ya Mei

Ligi kuu ya Ujerumani maarufu ,Bundesliga itarejelea mechi zake bila kuwa na mashabiki uwanjani tarehe 16 Mei.

Hiyo itakuwa mechi ya kwanza kuchezwa katika ligi la Ulaya kufuatia mechi nyingi kusitishwa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Moja ya michuano ambayo itachukua nafasi ni kati ya timu ya Schalke na Borussia Dortmund.

Mabingwa wa ligi hiyo Bayern Munich, ambao wanaongoza kwa alama nne kusawazisha kuingia kiwango cha juu, pale watakapokutana kwenye mechi mjini Berlin siku ya Jumapili.

Timu nyingi zina michezo tisa ya kucheza, na msimu huu fainali zinatarajiwa mwishoni mwa wiki ya tarehe 27-28 Juni.

Shirikisho la soka nchini Ujerumani (DFB) alisema msimu huu utaanza huku kukiwa na masharti ya kiafya ambayo lazima yazingatiwe kwa kutoruhusu mashabiki kuhudhuria uwanjani kuona mechi na wachezaji kupima virusi vya corona.

Watu wapatao 300 wakiwemo wachezaji, wafanyakazi na maofisa ndio watakuwa ndani au karibu na uwanja wa mpira, siku mechi itakapochezwa.

Ligi hii ilikuwa imesimasishwa tangu Machi 13. Vilabu vingi vilirejea kufanya mazoezi katikati ya mwezi Aprili, wachezaji wakiwa wanafanya mazoezi kwa makundi.

Christian Seifert, mkuu wa ligi la mpira wa mpira wa miguu nchini Ujerumani, alisema "imekuwa ni vigumu kurudia kucheza" licha ya kuwa wanacheza wenyewe na kuwepo kwa makatazo mengine.

Taarifa nyingine mpya ni pamoja na:

  • Kama ilivyo kwa wachezaji, makocha pamoja na waamuzi watafanyiwa vipimo pia na taratibu za usafi kuzingatiwa.
  • Hakuna ufafanuzi kuhusu matangazo ya mechi hizo kuwa yanalipiwa au bure nchini Ujerumani .Bado mazungumzo na mashirika ya utangazaji yanaendelea.
  • Kuna majibu ya watu 10 wenye virusi vya corona kutoka katika makundi makuu mawili kufuatia awamu ya kwanza ya vipimo vya corona, na wawili walikutwa katika awamu ya pili.

Jumatano wiki iliyopita Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alitangaza kupunguza baadhi ya nakatazo kwa kuruhusu maduka kufunguliwa baada ya watu wapatao 7,000 kufariki kutokana ns virusi vya corona.

Seifert alisema : "Mechi hizo zitahisi kuwa tofauti , baada ya mechi ya kwanza tutaelewa kwa nini tunapendelea mechi kuwa na mashabiki. Lakini kwa hali ilivyo inatubidi kujitahidi kufanya kile kinachowezekana kwa wakati huu."

Rais wa shirikisho la ligi la soka barani ulaya bwana Aleksander Ceferin alisema kuwa ana Imani kuwa Ujerumani itaweza kuonyesha mfano wa kuigwa duniani wa namna ya kurudi katika utekelezaji ukiachia changamoto zilizopo.

"Hii ni hatua kubwa nzuri ya kurejesha kwa watu maisha yaliyokuwa yamezoeleka. Haya ni matokeo ya mjadala ambao ulitathmini kwa kina na kupangwa kwa umakini kati ya mamlaka ya mpira wa miguu na wanasiasa," alisema.

Kwa kipindi hiki, kamati kuu la shirikisho la wachezaji duniani kuwasilisha 85,000 na wanariadhaa duniani kote, watakutana wiki ijayo kuja kuzungumzia masuala ya kuzingatia sheria za kiafya kufuatia kurejeshwa kwa michezo.

Katika maelezo yake: "Mapendekezo yote yatahitajika na matarajio ya wataalamu yatafikiwa huku wakijikita kuwa afya ya mchezaji sio kitu cha kufanyia mazungumzo, bali kufuata maagizo."

ADVERTISEMENT


Suala la uwepo wa mashabiki halipo

Union Berlin watachuana na leaders Bayern siku ya Jumapili wakati ligi zitakaporejea huku mchezaji Neven Subotic amekosoa jinsi hali hii inavyochukuliwa na mamlaka ya mpira wa miguu.

Soka la Ujerumani litaendelea licha ya kuwa ligi za Ufaransa, Netherland na Ubelgiji zimefungwa bado.

Subotic alisema kwenye kipindi cha mpira wa miguu cha BBC's World: "si salama kwetu sote kwa hali ilivyo. Hatutaweza kuja na ushindi mzuri , kutakuwa na masuala mengi ya kujikinga na hatari zozote zinazoweza kujitokeza na kufanya kile kilichozoeleka kwa kiwango kidogo.

"Tunaenda kucheza bila mashabiki na kwangu mimi jambo hilo linanifanye kuona are mchezo huu wa kipekee. Kucheza mpira wa miguu ni kitu cha kufurahia na huwa kigumu lakini kile ambacho kinafanya mchezo huu kuwa mzuri ni mashariki na jamii kwa ujumla.

"Hakuna kitu hapo na hakuna haja ya kuigiza kuwa si kitu kikubwa, mashabiki ndio nguzo kubwa ya mchezo kwa kuufanya uwe wa kipekee.

"Kitu ambacho nitafurahia ni mechi ya kwanza kurudi uwanjani pamoja na mashabiki kwenye uwanja.Ninasubiria kwa hamu siku hiyo ifike, hilo ndilo lengo langu la mwisho."Uchambuzi

Mechi hizi zinaoneka kuwa na muonekano tofauti, kusikika tofauti sana.Ni jambo la kuvutia kuwa hatimaye mechi za mpira wa miguu zinarejea kwa kati ya ligi bora ya soka duniani.

Bosi wa Ligi ya mpira wa miguu ya Ujerumani (DFL) Christian Seifert ametuma ujumbe wa tahadhari katika mkutano na waandishi wa habari, kusisitiza kuwa ukweli wa hali halisi kwa kusema "Tunacheza katika majaribio tu " na kuongeza kuwa wazo la afya na usafi linazingatiwa na linaweza kutekelezeka katika mechi.

Michuano ya timu za ndani kati ya waasimu Schalke na Borussia Dortmund ni njia nzuri ya kuanza lakini pia itaweza kuonyesha matokeo ya kukosekana kwa mashariki katika mechi kuendelea bila wao.

Premier League, La Liga na ligi zote zitakuwa zinaangalia namna mechi hizi za mwanzo zilivyocheza.Kama wataona Ujerumani imefanikisha kwa hilo kwa nini isiwe ulaya yote na hata ligi kubwa kuwa na fursa kubwa zaidi.

Jumamosi, Mei 16

Augsburg dhidi ya Wolfsburg

Borussia Dortmund dhidi ya Schalke

Eintracht Frankfurt dhidi ya Borussia Monchengladbach

Fortuna Dusseldorf dhidi ya Paderborn

Hoffenheim dhidi ya Hertha Berlin

RB Leipzig dhidi ya Freiburg

Jumapili , Mei 17

Cologne v Mainz

Union Berlin v Bayern Munich

Jumatatu, Mei 18.

Werder Bremen v Bayer Leverkusen

ADVERTISEMENTPost a Comment

0 Comments