tangazo

Madereva wa Tanzania wagoma kupimwa corona kwenye mpaka wa Horohoro

Ripoti za corona zilizoripotiwa na ‘The Citizen’ na ‘Daily Monitor’ zinasema baadhi ya Madereva wa Tanzania wamegoma kupimwa corona kwenye mpaka wa kuingilia Kenya wa Horohoro bila usimamizi wa Madaktari kutoka Tanzania kwa kile kinachoonekana wamekosa imani na Madaktari Wakenya kwakuwa vipimo vyao vimekuwa vikionesha wengi wao kuwa na corona.

Utaratibu wa Mamlaka za Kenya kuwapima Madereva mpakani kabla ya kuingia nchini mwao, umesababisha Madereva wengi kusubiri kwa muda mrefu mpakani, Namanga pekee wamerekodiwa zaidi ya Madereva Malori 300 wanaosubiri vipimo.

Wizara ya Afya Kenya juzi ilitangaza kuwa Madereva wa Malori wawili kutoka Tanzania wamebainika kuwa na corona na kurejeshwa Tanzania huku ripoti mpya ya Wizara hiyo ya Afya Kenya ikisema Madereva wengine 25 kutoka Tanzania nao wamebainika kuwa na corona na kurejeshwa pia Tanzania.

Post a Comment

0 Comments