tangazo

MAFURIKO DSM: Nyumba zimezama, mtumbwi watumika kuvusha Watu “wengine wamekimbia, wengine wanahangaika”

Wakazi wa kaya zaidi ya 20 eneo la Pugu, DSM wamelazimika kuyakimbia makazi yao , baada ya mafuriko kuzikumba nyumba zao na kuharibu mali , nyumba zimezama na kujaa maji hadi kufanya wakazi hao kutumia mtumbwi  kutoka eneo moja hadi jingine mtaani hapo.
“Wananchi wanateseka, wengine wamepanga, wengine wamehifadhiwa kwa Ndugu na Wasamaria wema lakini Wapo wanaodansi tu hawana pesa hawajui wapi pa kwenda, Watu wa mazingira wamekuja hapa lakini hatujapata majibu rasmi, tumeshalifikisha ngazi za juu hili”– Amanzi Bungara, Mwenyekiti wa Mtaa

LIVE MAGAZETI: WABUNGE CHADEMA WAKIMBIA CORONA BUNGENI, MSHTUKO KIFO CHA BALOZI MAHIGA

Post a Comment

0 Comments