Mahakama kuu Marekani yaanza kusikiliza kesi kuhusu nyaraka za kodi za Trump

Mahakama ya juu nchini Marekani Jumanne hii inaanza kusikiliza kesi kubwa ya kisiasa dhidi ya rais Donald Trump kukataa kuwasilisha nyaraka za ulipaji kodi na rekodi za kifedha kwa bunge na mwendesha mashitaka wa New York, kesi ambayo inaweza kuamua ukomo wa kinga ya urais.

 Majaji tisa wa mahakama ya juu ambao wapo nyumbani kwa sababu ya janga la corona, watawahoji mawakili wa pande mbili kwa njia ya simu na kurushwa moja kwa moja kupitia televisheni.

 Hukumu hiyo ya mahakama ambayo inatarajiwa kabla ya mwisho wa mwezi wa sita, itawaruhusu majaji kutoa maamuzi kabla ya uchaguzi wa mwezi Novemba ambapo Trump anatafuta muhula wa pili madarakani.

 Trump anakuwa rais wa kwanza tangu Richard Nixon katika miaka ya 70 kukataa kutoa nyaraka zake za ulipaji kodi na hivyo kuibua uvumi juu ya thamani halisi ya utajiri wake na uwezo wake wa kifedha.

ADVERTISEMENT

Post a Comment

0 Comments