Majaji 125 kutoka mabara manne wajadiliana kutumia Tehama kukwepa corona

MAJAJI 125 kutoka katika mabara manne wamefanya mkutano kwa njia ya mtandao kujadili jinsi ya kuendelea na shughuli za ma- hakama kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHA- MA) ili kuepuka maambukizi ya virusi vya corona.

Mkutano huo uliandaliwa na Shirika la Miliki Bunifu Duniani (WIPO) ambalo liko chini ya Umoja wa Mataifa (UN)

Akizungumza kuhusu mku- tano huo, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Bi- ashara, Stephen Magoiga, alisema ulishirikisha majaji kutoka Afrika, Ulaya, Marekani na Asia.

Tanzania jaji Magoiga na mwakilishi wa WIPO kutoka Mahakama ya Tanzania, ambaye ni Hakimu Mkazi na Msaidizi wa Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Upendo Ngitiri.

Jaji Magoiga alisema miongoni mwa waliyopendekeza katika mku- tano huo, ni majaji kuwezeshwe kuwa na huduma ya mtandao (internet) nyumbani na sio ofisini tu. “Suala la mabadiliko ya Tehama ni muhimu ili tuendane na mab- adiliko ya teknolojia. Hivyo Majaji wasiwe na huduma ya mtandao maofisini tu bali hata kwenye nyumba zao ili waweze kuendelea

na huduma za utoaji haki hasa katika kipindi hiki cha janga la co- rona hata wakiwa nyumbani kwa kuwa wakati mwingine hawawezi kumaliza kazi ofisini, pia itawawez- esha kufanya tafiti mbalimbali,” alisema Jaji Magoiga.

Jaji Magoiga alisema kupitia mkutano huo, wamejifunza kuwa majaji wa Uingereza mazingira yao yanawaruhusu kufanya kazi hata wakiwa nyumbani kwa mu- jibu wa Jaji wa Mahakama Kuu ya Uingereza, Collins Birss.

Aliongeza kwamba matumizi ya Tehama pia yanasaidia kulinda usalama wa watumishi katika kip- indi hicho na kutoa huduma kwa gharama nafuu.

Naye Ngitiri alisema katika mkutano huo, wamejifunza kwam- ba huduma za utoaji haki zinaweza kuendelea kutolewa kwa njia ya mawasiliano ya simu kwa nchi am- bazo zimewekewa zuio la kutotoka nje ikiwa ni hatua za kukabiliana na virusi vya corona, kupitia Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Mare- kani, Cathleen Malley.

WIPO ilifanya mkutano
wa siku saba nchini Tanzania mwaka jana katika Hoteli ya
Hyatt Regency jijini Dar es Salaam ulioshirikisha washiriki 35 kutoka nchi za Sweden, Switzerland, Ne- pal, Cambodia, Rwanda, Uganda, Mozambique, Zambia, Mala

Post a Comment

0 Comments