tangazo

Majibu ya Silinde kuhusu kuhama CHADEMA

Mbunge wa Jimbo la Momba David Silinde, amesema kama atahitaji kufanya maamuzi ya kuhama CHADEMA wakati ukifika atazungumza, lakini kwa sasa yanayozungumzwa ni maoni ya watu hawezi kuwaingilia.

Silinde ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika kipindi cha #SupaBreakfast ya East Africa Radio, Silinde amesema kama Mbunge ana mipango mirefu kwenye siasa kama ilivyo kwa baadhi ya Viongozi wengine wa upinzani.

"Sijatangaza uamuzi wa kuhama, yanayosambazwa ni maoni ya watu na mitazamo, mimi bado ni Mbunge wa CHADEMA na kiongozi wa CHADEMA, kama kuna tamko lolote nitalitoa wakati utakapofika." amesema Silinde.

"Mazungumzo yanayoonekana mtandaoni kuwa si malengo yangu kuwa upinzani ni kweli ni yangu, Mwanasiaa yeyote lazima awe na malengo, ndiyo maana Diwani atatamani kuwa Mbunge, Mbunge atatamani kuwa Waziri na Waziri atatamani kuwa Rais" ameongeza Silinde.

Post a Comment

0 Comments