tangazo

Mali za ndugu wa Rais wa zamani wa Sudan kutaifishwa

Kamati ya kapambana na rushwa nchni Sudan imesema itataifisha maeneo makubwa ya ardhi na nyumba za makaazi zinazomilikiwa na ndugu wa rais aliyeondolewa madarakani Omar al-Bashir.

Kamati hiyo imesema uamuzi huo umefikiwa baada ya uchunguzi kubaini umiliki wa mali hizo ikiwemo ardhi yenye ukubwa wa mita za mraba 92,000 ulitokana na mahusiano ya kifamilia.

Sehemu ya wanaomiliki mali hizo inajumuisha shemeji wa al-Bashir, wapwa na binamu zake pamoja na waziri wa zamani wa Ulinzi aliyekuwa mshirika wa karibu wa rais huyo wa zamani.

 Katika hatua nyingine kamati hiyo imezivunja bodi za kampuni mbili za uendeshaji uwanja wa ndege wa kimataifa wa Khartoum kutokana na madai ya rushwa.

Kamati hiyo iliyoundwa na mwanasheria mkuu wa serikali inasimamia uchunguzi wa makosa yanayohusu fedha za umma na rushwa yaliyofanywa na al-Bashir, ndugu zake na washirika wa utawala wake.

Post a Comment

0 Comments