Malkia Elizabeth kuongoza kumbukumbu za miaka 75 ya kumalizika vita vya pili vya dunia

Malkia Elizabeth wa II leo atatoa hotuba kwa njia ya televisheni kuadhimisha miaka 75 tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia huku sherehe za mwaka huku zikiandamwa na kiwingu cha janga la virusi vya corona.

Hotuba ya Malkia Elizabeth itakuwa ishara muhimu inayotolewa miaka 75 tangu baba yake Mfalme George wa VI alipolihutubia taifa kwa njia ya redio na kutangaza ushindi katika vita kuu vya pili vya dunia.

Matukio kadhaa yaliyopangwa kusherehea siku ya ushindi wa majeshi ya nchi washirika dhidi ya manazi wa Ujerumani yamefutwa baada ya serikali kupiga marufuku ya mikusanyiko kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.

Hata hivyo tukio la kurushwa kwa ndege za kivita litafanyika kama kawaida na waziri mkuu Boris Johnson atazungumza na maveterani kwa njia ya video pamoja na kutoa ujumbe wa kuadhimisha siku hiyo ya kitaifa

Post a Comment

0 Comments